Maoni ya Mheshimiwa Mbunge Ally Mohamed Keissy (CCM, Nkasi) akitoa maoni yake kuhusu 'mzigo' wa Muungano wa Tanzania kwenye Bunge Maalum la Katiba ambapo Wajumbe kadhaa hasa wa kutoka Zanzibar walipaza sauti kusema kuwa 'anatukera' kwa kauli za maudhi.
Keissy alikejeliwa kuwa mwenyewe ni 'Mpemba', 'Mmanga', 'Mwarabu', 'Mgonjwa wa akili akapimwe', na kadhalika na kushauri kuwa kwa nini asirudi kwao Uarabuni akapimwe, huku akirukia akisema anayemsema naye ni 'Mkongomani'.
Hii si mara ya kwanza kwa Mhe. Keissy kukera Wazanzibari, tunaweza kubofya hapa kurejea kero ya mwezi Mei.

إرسال تعليق