Kukiwa
na wanawake warembo katika magari yanayomeremeta, waliovikwa na nguli
wa mavazi Ally Rhemtulla kwa ajili ya kupokea wageni kwenye hafla ya
kuona mashindano ya magari ya Formula One iliyoandaliwa na kampuni ya
CFAO Motors kwa mashabiki wa mchezo huo na wateja wake.(Picha zote na
Zainul Mzige).
Na Mwandishi wetu
JUMAPILI
wakati kiwanja cha mbio za magari za Formula One cha Monza Italia
kinawaka moto, wapenzi wa mchezo huo jijini Dare s salaam walipata
uhondo wa kuona mkali wa injini na udereva, katika skrini kubwa
iliyowekwa makao makuu ya CFAO Motors Tanzania, Barabara ya Nyerere,
Dare s salaam.
Katika
hekaheka hiyo iliyochukua takribani saa moja na kumaliza lap zote 53
mchuano mkali ulikuwa kwa timu ya Merceders Benz ambapo gari zake mbili
zikiendeshwa na Hamilton na nyingine Rosberg zilichuana vikali.
Wakiandaa
kwa mara nyingine hafla ya kuona mashindano ya magari ya Formula One,
CFAO Motors iliwapeleka Watanzania na wageni waliokusanyika hapo Italia
kwa staili ya aina yake na gemu ilipoanza ilikuwa mshikemshike.
Wakati
watanzania hao wakisubiri majira ya Italia ya kuanza kwa mchuano huo,
walipata burudani kutoka kwa madame Emilie na Madame Otilie kwa dansi la
nguvu ambalo liliwaacha wageni waalikwa na miguno ya raha.
Wageni wakipokelewa na wafanyakazi wa CFAO Motors wakati wa halfa hiyo.
Huku
vinywaji na vitafunwa vikiendelea katikia ukumbi uliosukwa vyema na
Irene wa DSM Treasue, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors,
Bw.Wayne McIntosh, alielezea hafla yake na maana kwa timu nzima CFAO
Motors Tanzania ambao ndio wawakilishi pekee wa Mercedes Benz.
Alisema
ni hafla iliyolenga kuwaleta pamoja wapenzi wa mchezo na wadau
wengine wa CFAO Motors kama sehemu ya kujuana na kuona mali mpya
iliyoingia sokoni kwa lengo la kuwasaidia Watanzania kujiamini zaidi.
Alisema
mwaka huu wamezindua kitu kipya mtaani cha S-Class ambacho ubora wake
ni matokeo ya kazi kubwa ya Mercedes katika kuhakikisha inawapatia
wananchi na wateja wake kitu bora zaidi.
Kukiwa
na wanawake warembo katika magari yanayomeremeta, waliovikwa na nguli
wa mavazi Ally Rhemtulla tukio la kuangalia mchuano wa timu mbalimbali
za magari , kama ilivyokuwa ikitokea Monza lilijaa ushababi wa aina yake
uoliofanya wengi waliofika kuifurahia Jumapili yao.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh akisoma risala
kwa wageni waalikwa kwenye hafla ya kuona gemu ya mashindano ya magari
ya Formula One iliyoandaliwa CFAO Motors usiku wa kuamkia leo jijini
Dar.
Kama
ilivyotokea Monza, Italia ambapo Lewis Hamilton alipambana vikali kuwa
katika fomu baada ya kuanza vibaya kipenga kilipoanzisha mbio na baadae
kushika usukani , kushinda na kumwagiwa shampeni, bahati nasibu ndogo
iliyochezeshwa CFAO Motors baada ya mbio zile iliwapatia shampeni na cha
juu Kamili Delaware kama mshindi wa kwanza, akifuatiwa na Kauthar
Mukhtar na wa tatu MaCarrie Dickin.
Tukio
la kuangalia mashindano ya magari ya Monza liliongezwa nakshi na
Tanzania Breweries kwa vinywaji vyao, MMI pia kwa vinywaji ambapo pia
waliwapa nafasi wadau kuonja Patron tequila na Azam ambao walileta
vinywaji na vipozo koo vya washangiliaji, ashkrimu.
CFAO
wakitumia tukio hilo kuonesha pia bidhaa zao mpya walikuwa na kila
sababu za kuelezea ubora wa magari ya Mercedes Benz ma huduma zake
kuanzia magari ya familia hadi malori makubwa ya kibiashara, hasa baada
ya timu za Mercedes benz kutwaa ushindi katika mashindano ya Monza.
Mshindi
wa pili alikuwa Nico Rosberg (wa Mercedes pia) ambaye alishindwa
kuhimili presha kubwa aliyokuwa akipumuliwa na Hamilton katika mbio
hizo.
Ilikuwa
ni katika lapu ya 29 wakati Rosberg, alipofanya kosa lililompokonya
pointi 22 katika mbio za kuwania ubingwa wa Formula One.
Pichani
juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa wakimsikiliza Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh (hayupo
pichani).
Pamoja
na hilo Mercedes ilishangilia kutokana na kuwa na nafasi mbili za
ushindi ambazo hawajawahi kuzipata tangu tukio la Austria Juni mwaka na
sasa wamepata ushindi wa saba katika michuano 13 iliyokwishafanyika.
Aliyeshika namba tatu ni Mbrazil Felipe Massa akiwa katika timu ya Williams inakuwa ni ushindi wake wa kwanza tangu mei 2013.
Rosberg,
ambaye sasa anapointi 238 dhidi ya 216 za Hamilton huku ikibaki
michuano 6 ya bara la Ulaya katika mahojianoi alikiri kosa lakini
akasema kwamba Lewis alikuwa na kasi kubwa.
“Unajisikia
vibaya kupoteza ushindi namna ile, lakini Lewis alikuwa na kasi kubwa
katika mchezo mzima.Alikuwa anakuja kama roketi na ilikuwa lazima
nijisukume zaidi,kisha likaja kosa,” alisema.
Kuanza vibaya kwa Hamilton kulitokana na tatizo la kiufundi katika gari lake baada ya kuchelewa kuanzisha mfumo.
Bottas
katika michuano hiyo alishika nafasi ya nne baada ya kufanya kazi ya
akili ya kuyapita mgari mengine hasa baada ya kuchemsha katika lapu ya
kwanza ambapo aliimaliza akiwa wa kumi.
Dereva
wa Ferrari, Fernando Alonso alilazimika kuondoka nje ya mashindano
kwenye lapu ya 29 baada ya gari lake kupata hitilafu kwenye mfumo wa
nishati, ikiwa ni mara ya kwanza kukumbwa na tatizo la aina hiyo katika
mbio 86 alizoshiriki mpaka sasa na Kimi Raikkonen alimalizia wa tisa.
Mfiniland
huyo alimalizia akiwa wa kumi lakini alipanda baada ya dereva wa
McLaren, Kevin Magnussen kuchapwa penati kwa kumuondoa barabarani
Bottas .
Hadi Jumapili hii, Alonso ni dereva pekee ambaye amekuwa akipata pointi katika kila mbio.
Wadau wa CFAO Motors na mashabiki wa mashindano ya magari ya Formula One wakila pozi.
MuAustralia,
Daniel Ricciardo, ambaye amshinda mbio nyingine mbili za awali, alikuwa
na siku nzuri na timu yake ya Red Bull kwa kumalizia wa tano. Kazi ya
kuyapita magari mengine aliyafanya katika hali ya mshangao mkubwa
akiwapita madereva mbalimbali akiwemo Sebastian Vettel (mshindi mara
nne) ambaye alimalizia wa sita.
Mmexico
Sergio Perez alikuwa wa saba akifanyia kazi timu ya Force India
kibarua kizito kwa jinsi walivyokuwa wanagombvania nafasi yeye na dereva
wa timu ya McLaren, Jenson Button ambaye alishika nafasi ya nane.
Kwa mujibu wa Mtangazaji michuano hiyo sasa inaelekea viwanja vya Mashariki ya mbali vya Singapore na Japan.
Karen
Emilie Asla (kushoto) na Anette Otilie Pettersen kutoka Maendeleo Dance
Group wakitoa burudani kwa wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo.
Meneja Masoko wa CFAO Motors, Tharaia Ahmed (mwenye sketi ya kijani) akifurahi jambo na baadhi ya wageni waalikwa.
Karen
Emilie Asla kutoka Maendeleo Dance Group akichagua namba za bahati
nasibu iliyochezeshwa maalum kwa wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya
kuona gemu ya mashindano ya magari ya Formula One iliyoandaliwa CFAO
Motors kwa ajili ya wateja wake na wadau mbalimbali ambayo imefanyika
makao makuu ya ofisi za kampuni hiyo. Wa tatu kushoto ni Meneja Masoko
wa CFAO Motors, Tharaia Ahmed na Wa pili kushoto ni MC Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh. Kulia ni
Mwakilishi kutoka kampuni ya mmi Tanzania (Maritime and Merchantile
International Tanzania Ltd.) ambao ni wauzaji na wasambazaji wa vinywaji
vikali na mvinyo.
Meneja
masoko kwa kampuni ya CFAO Motors, Tharaia Ahmed (wa tatu kulia)
akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wageni waalikwa aliyeibuka mshindi wa
tatu MaCarrie Dickinson (wa pili kulia) kwenye bahati nasibu hiyo.
Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne
McIntosh.
Meneja
masoko kwa kampuni ya CFAO Motors, Tharaia Ahmed akikabidhi zawadi
kwa mshindi wa pili wa bahati nasibu hiyo Bi. Kauthar Mukhtar(katikati).
Meneja
masoko kwa kampuni ya CFAO Motors, Tharaia Ahmed akikabidhi zawadi
ikiwemo chakula cha usiku kwa watu wawili kwenye hoteli ya Hyatt Regency
– The Kilimanjaro mshindi wa kwanza Bw. Kamil delaware (kulia)
huku Mwakilishi kutoka kampuni ya mmi Tanzania (Maritime and Merchantile
International Tanzania Ltd.) ambao ni wauzaji na wasambazaji wa
vinywaji vikali na mvinyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh ( katikati)
akitoa shukrani kwa wageni waalikwa na wadhamini waliofanikisha sherehe
hiyo wakati wa hafla ya kuona mashindano ya Formula One kupitia Big
screen kubwa iliyowekwa ukumbini hapo kwenye makao makuu ya ofisi za
CFAO Motors jijini Dar.
Pichani
juu na chini ni baadhi ya wateja na wadau wa CFAO Motors wakishuhudia
mashindano ya Formula One kupitia Big screen iliyokuwepo ukumbini hapo
kwenye makao makuu ya ofisi hizo.
Wageni waalikwa wakijipatia vinywaji mbalimbali vikiwemo vinywaji vya Azam.
Mvinyo
na vinywaji vikali kutoka kampuni ya mmi Tanzania (Maritime and
Merchantile International Tanzania Ltd.) navyo vilikuwepo.
Muhudumu akiwasikiliza wageni waalikwa kwenye huduma za vinywaji.
Mhasibu
Mkuu wa Kampuni ya CFAO Motors Bw. Aldo Pagan (kulia) akibadilishana
mawazo na baadhi ya wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo.
Tender
Manager wa CFAO Motors Bw. Marco Kahabi (wa pili kulia) akisalimiana na
mmoja wa wageni waalikwa. Kulia ni Meneja Masoko wa CFAO Motors,
Tharaia Ahmed.
Kinywaji kikali aina ya PATRON kinachosambazwa na kampuni ya mmi Tanzania.
Meneja masoko kwa kampuni ya CFAO Motors, Tharaia Ahmed akiteta jambo na mmoja wa wageni waalikwa kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Hoteli ya Golden Tulip, Bw. Aatish Ladwa.
Wageni waalikwa walipata fursa ya kunywa na kubadilishana mawazo kama wanavyoonekana pichani.
Mdau kutoka kampuni ya Azam (kulia) akipata picha ya kumbukumbu na wadau.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh (wa pili
kushoto) na Meneja masoko kwa kampuni ya CFAO Motors, Tharaia Ahmed
wakipata picha ya kumbukumbu na wageni waalikwa.
Mkurugenzi
wa kampuni ya mmi Tanzania (Maritime and Merchantile International
Tanzania Ltd.) ambao ni wauzaji na wasambazaji wa vinywaji vikali na
mvinyo, Bi. Stephi Hill Said (kulia) akifurahi jambo na marafiki zake
wakati wa halfa hiyo.
Wadau wa CFAO Motors wakila pozi kwenye gereji ya kufanyia matengenezo magari ya wateja wa kampuni hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh akifurahi jambo na wadau wa CFAO Motors.
Wageni waalikwa wakijinoma Ice Cream za Azam ambao walikuwa ni mmoja wa wadhamini wa hafla hiyo.
Wageni waalikwa wakinywa na kufurahi.
Mwakilishi
wa kampuni ya mmi Tanzania (Maritime and Merchantile International
Tanzania Ltd.) ambao ni wauzaji na wasambazaji wa vinywaji vikali na
mvinyo (kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya wageni waalikwa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh akibadilishana
mawazo na baadhi ya wageni waalikwa kwenye hafla hiyo.
Meneja Masoko wa CFAO Motors, Tharaia Ahmed (wa tatu kushoto) katika picha ya pamoja na wageni waalikwa.
Meneja Masoko wa CFAO Motors, Tharaia Ahmed katika pozi na wafanyakazi wenzake.




































Post a Comment