Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo 'CHADEMA' na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe,
Na Ojuku Ibrahim
MAAZIMIO ya Mkutano Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya kuitisha maandamano na migomo isiyokoma nchi nzima kupinga kuendelea kwa vikao vya Bunge Maalum la Katiba (BMK) na baadaye kauli kali ya Jeshi la Polisi ya kukataza kitendo hicho na kutishia kutumia nguvu kuyazima, yanaweza kusababisha maafa kama busara hazitatumika kwa pande zote mbili.
MAAZIMIO ya Mkutano Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya kuitisha maandamano na migomo isiyokoma nchi nzima kupinga kuendelea kwa vikao vya Bunge Maalum la Katiba (BMK) na baadaye kauli kali ya Jeshi la Polisi ya kukataza kitendo hicho na kutishia kutumia nguvu kuyazima, yanaweza kusababisha maafa kama busara hazitatumika kwa pande zote mbili.
Hayo
yamesemwa na baadhi ya wananchi wa kada na vyama mbalimbali waliohojiwa
kufuatia kuitwa polisi na kuhojiwa kwa Mwenyekiti wa Chadema Freeman
Mbowe aliyetoa kauli hiyo wakati wa mkutano wa chama hicho hivi
karibuni.GPL
Chacha
Maiya, aliyejitambulisha kama mwanafunzi wa sheria kutoka Chuo Kikuu
Huria, alisema ingawa ni haki ya msingi kwa wananchi kuandamana, lakini
tafsiri inayotokana na maneno ya Mbowe ni kama inayoashiria vurugu
kutoka kwa wafuasi wake, jambo ambalo halikubaliki.
“Ni kama
vile Mwenyekiti Mbowe anawahamasisha wafuasi wake kufanya vurugu.
Nadhani kulikuwa na haja ya kuwa makini katika kutoa matamshi hasa
unapotaka kuhamasisha umma, sasa suala la msingi ni kwa wao kusitisha
maandamano yao na kufikiria njia nyingine ya kuwasilisha ujumbe wao kwa
Rais au Bunge,” alisema.
Akizungumzia
sakata hilo, kiongozi mmoja wa Chadema aliyeomba hifadhi ya jina lake,
alisema kitendo cha polisi kuzuia maandamano yao hakiwezi kulipa uhalali
Bunge Maalum kuendelea, isipokuwa wanazidi kuchochea ari ya wananchi
katika kutafuta haki yao.
“Ipo siku
watu watasema basi, imetosha, hivi vitisho vina mwisho wake, polisi
wanataka kuingilia siasa kwa kuilinda CCM, lakini watambue kuwa hakuna
sheria inayowapa mamlaka ya kuzuia maandamano ya kisiasa, walichopaswa
kufanya, ni kutoa maelekezo ya namna ya kufanikisha maandamano hayo ili
yatawaliwe na amani, siyo kupiga watu mabomu,” alisema.
Tokea
kutolewa kwa maazimio hayo ya Chadema, wafuasi kadhaa wa chama hicho
wamekamatwa katika maeneo mbalimbali nchini na wengine kufikishwa
mahakamani, baada ya kujaribu kuandamana na polisi kutumia nguvu
kuwazuia
إرسال تعليق