DENTI wa Chuo cha Ubaharia (EMI) kilichopo Posta
jijini Dar, Alpha Mohamed (18) aliyedaiwa kupigwa na Diwani wa Kata ya
Sinza kwa ‘leseni’ ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Renatus Pamba, ‘Mr Simple’, bado yu hoi katika Hospitali ya
Mwananyamala, Dar.
Alpha alidaiwa kupigwa Agosti 29, mwaka huu nyumbani kwa diwani huyo
Sinza- White Inn, Dar ambapo chanzo cha kipigo hicho kilisemekana kuwa
ni denti huyo kukutwa akipiga stori na binti wa diwani aliyejulikana kwa
jina moja la Mage.
Ilidaiwa kwamba baada ya vipimo ilibainika kwamba denti huyo alipata
maumivu makali kifuani na mgongoni baada ya kupigwa na fimbo pamoja na
fagio.
Chanzo chetu kilibaini licha ya Alpha kupelekwa katika Hospitali ya
Palestina iliyopo Sinza jijini Dar lakini hali ilizidi kuwa mbaya kwani
mara kwa mara amekuwa akitapika damu na kulalamika kupata maumivu makali
maeneo ya kifua na kichwani huku akikohoa damu.
Ilisemekana kwamba kutokana na hali kuzidi kuwa mbaya, ndugu wa Alpha
wamelazimika kupitisha karatasi ya michango mtaa mzima kumchangia fedha
za matibabu ili kunusuru maisha yake.
Alipotafutwa mjomba wa Alpha, Aboubakari Ramadhani ili kujua afya ya Alpha, alisema bado haijatengemaa na amelazwa Mwananyamala.
Alipotafutwa mjomba wa Alpha, Aboubakari Ramadhani ili kujua afya ya Alpha, alisema bado haijatengemaa na amelazwa Mwananyamala.
“Hali yake ni mbaya, hatujui nini kitatokea. Familia ilifungua jalada
la kesi lenye kumbukumbu KN/RB/7748/2014 SHAMBULIO hivyo tunaendelea
kumtibu huku tukisubiri hatua za kisheria,” alisema Ramadhani.Baada ya
habari ya tukio hilo kuripotiwa kwenye gazeti hili toleo Na 1145 lenye
kichwa cha habari kilichosomeka;
DIWANI AMPA KIPIGO DENTI, wanahabari wetu walimtafuta diwani huyo ili
kujua undani wa sakata hilo kwani naye alifungua mashitaka akidai Alpha
alimbaka bintiye, lakini hakutoa ushirikiano.
Kwa nyakati tofauti, sakata hilo limeripotiwa katika vituo viwili tofauti vya polisi, Kijitonyama-Mabatini alikoshitakiwa diwani na Urafiki-Ubungo ambako diwani alimshitaki Alpha akidai alimbaka bintiye, Mage.
Kwa nyakati tofauti, sakata hilo limeripotiwa katika vituo viwili tofauti vya polisi, Kijitonyama-Mabatini alikoshitakiwa diwani na Urafiki-Ubungo ambako diwani alimshitaki Alpha akidai alimbaka bintiye, Mage.
إرسال تعليق