Na Magreth Kinabo, Dodoma
Mwenyekiti wa Chama cha UPDP
Taifa , na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Fahmi Dovuta amesema
anawashangaa viongozi wanaojiita UKAWA kwa kumwita msaliti, huku
akihoji kwamba anawezaje kukihujumu chama chake na vinginneyo.
Kauli hiyo ilitolewa leo na
Mwenyekiti huyo mjini Dodoma wakati kikao cha Thelasini na Tisa cha
Bunge hilo, linaloendelea mjini huo kujadili sura za Rasimu Mpya ya
Katiba zilizobakia na sura mpya.
“ Nimepokea simu mara tatu za vitisho, kwamba watanifanyizia.
“ Wenzetu hawa kama walikuwa
hawakubaliani , walikuwa na nafasi ya kuomba mashauriano halafu
wakesema hayo wanayoyasema,” .alisema Dovutwa.
Aliongeza kuwa katika kikao cha
Viongozi Wakuu wa Vyama vya Siasa vyenye wabunge vinavyounda Kituo
cha Demokrasia nchini(TCD) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete .
Dovutwa ambaye ni mwakilishi wa
vyama vya siasa visivyokuwa na wabunge Bungeni, alifafanua kwamba
katika kikao hicho, cha Septemba 8, mwaka 2014 mambo waliyokubaliana
ni kwanza kufanya marekebisho kuhusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na
kuhusu usitishwaji wa Bunge hilo, hakuna mwenye mamlaka kisheria.
Aliendelea kuelezea kuwa
katika kikao cha Agosti 31, mwaka 2014 Tundu Lissu alimtaka Rais
Kikwete kusitisha Bunge hilo, lakini Rais Kikwete akamjibu yeye ndiye
aliyetaka (Rais) asiwepo katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, huku
akimhoji kuwa amwonyeshe sheria atakayoitumia.Aliongeza kwamba Lissu
hakuwa na la kusema.
Dovutwa alisema walikubaliana
kwamba waje katika Bunge hilo, lakini wanaona kuganyaga mlango wa wa
Bunge hilo ni ugumu kama kurudia ‘kunyonya, kama hawataki kuzungumza
mbele ya wenzetu… nani wa kulaumiwa,’ alisisitiza.
Aidha Dovutwa alisema katika
mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika hivi karibuni, ilikuwa
viongozi hao na waje kwa ajili ya kutoa tamko la kuhusu makubaliano
ya kikao hicho, lakini hawakutokea.
“Hili ni jambo baya linaleta chuku na uchonganishi wa halai ya juu,” alisema Dovutwa.
Akizungumzia kuhusu suala la
kukataa kusaini , alisema walijua ilikuwa ni mtego kwa vile walipewa
maelezon wasaini dakika chache kabla ya kuingia katika kikao hicho,
hivyo hawakuwa na muda wa kusoma.
Alisema pia walibaini kuna kipengele cha hatari cha kutaka Bunge lisitishwe.

Post a Comment