Msanii kutoka Kigoma, anayefanya vizuri na wimbo wake ‘Wema Kwa
Ubaya’, Linex aka Mjeda amesema wimbo huo ni mkubwa kutokana na ujumbe
ulioubeba.

Linex amesema hana desturi ya kusikiliza nyimbo zake, lakini kutokana
na ujumbe wa ‘Wema kwa Ubaya’ amekuwa akifanya hivyo mara kwa mara.
“Unajua wimbo wangu wa sasa ‘Wema Kwa Ubaya’ umefanya vizuri haraka
nahisi kutokana na muziki ambao nimefanya una ujumbe kwa jamii,” amesema
Linex. “Unajua sasa hivi watu wengi wanaimba mapenzi. Wimbo upo tofauti
sana, maana sometimes hata mie mwenyewe huwa huu wimbo unanichukua muda
mwingi sana, hasa pale ninapousikiliza. Unajua huwa sina taratibu ya
kusikiliza ngoma zangu, lakini hii nimekuwa nikisikiliza sana.”
“Huu wimbo nilirekodi miaka mitatu iliyopita. Kwahiyo huu ulikuwa ni
muda wake wa kutoka. Lakini huu wimbo, baadhi ya maneno alinipa
mheshimiwa Zitto Kabwe. Pia idea ya huu wimbo ilitoka kwenye wimbo wa
Aifora, kuna mstari unasema ‘siwezi kukuvua wema na kukulipa mabaya’.
Mheshimiwa Zitto akanimbia ‘unajua hilo neno unaweza kupata wimbo ambao
utajitegemea’ akaniambia ‘chukua maneno ya Wema badala ya Mabaya, weka
kwa ubaya ndo ikawa “Wema Kwa Ubaya”.
Linex amedai kuwa kwa sasa anaandika filamu yenye jina la ‘Wema kwa Ubaya’ na wimbo utakaofuata ni ule aliomshirikisha Diamond.
“Sasa hivi naandika movie ya ‘Wema kwa Ubaya’ ambayo nitawapa watu
wengine wafanye. Pia kuna ngoma itakuja baada ya hii ‘Wema kwa Ubaya’
nimefanya na Diamond inaitwa ‘Salima, kwahiyo sasa hivi mashabiki wangu
wategemee ngoma baada ya ngoma hakuna kulala.
Linex alizungumzia pia uhusiano na msichana wa kizungu ambaye
inasemekana waliachana. “Unajua hatukuachana, sema tulikuwa kidogo kuna
vitu tumetofautiana lakini sasa hivi tupo sawa na alikuwa Dar hivi juzi,
lakini ameondoka tena.”
إرسال تعليق