Gari aliyokuwa amepanda MAALIM SEIF ikiwa imeharibika vibaya
Habari zilizotufikia mda huu
Zinasema MSAFARA wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya mapinduzi ya
Zanzibar na Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif
Sharif Hamad umepata Ajali mbaya Mkoani Mwanza na kupelekea Viongozi
mbalimbali wa Chama hicho kuwa na hali mbaya.
Vilevile Mkurugenzi huyo wa Habari
wa Chama hicho alisema kwa sasa Majeruhi hawo wamekimbizwa kwenye
Hospitali ya Bugando kupatiwa matibabu na hali yao inaendelea vizuri
isipokuwa Katibu chama cha Cuf kutoka Wilaya ya Nyamagana Rehema Mwenda
hali yake sio Nzuri kutokana na kupoteza Fahamu
Mkurugenzi wa habari wilaya’na MH SHIDO Ambae ni mwenyekiti wa serikal ya mtaa uliyopo kata ya miringo,wameumia vibaya wamelazwa hospitali ya BUGANDO
Akithitisha kutokea kwa Ajali
hiyo wakati anaongea na Mwandishi wa Mtandao huu, mda huu kwa njia ya
simu kutoka Mkoani Mwanza kwenye Ajali hiyo, Naibu Mkurugenzi wa Habari
kutoka Chama cha Wananchi CUF bwana Kambaya alithibitisha kutokea kwa
Ajali hiyo na kusema Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya mapinduzi
ya Zanzibar Maalim na Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF) Seif
Sharif Hamad ajadhurika na yuko salama bali waliodhurika na Ajali hiyo
ni viongozi wa chama hicho,

| Rehema Mwenda alikuwa kwenye msafara huo akiugulia maumivu |
“Ni kweli Msafara wa Makamu wa
rais na Katibu mkuu Taifa umepata ajali ila yeye yuko salama,lakini
viongozi wetu wa chama akiwemo katibu wa Chama cha Wananchi CUF Wilaya
ya Nyamagana Be Rehema Mwenda Pamoja na Mkuu wa Kitengo cha cha Habari
wa chama Chetu wilaya ya nyamagana Hassan Shido ndio wamepata majeraha
kutokana na Ajali hiyo,”alisema Kambaya.
Kambaya alizidi kusema Ajali
imetokana na Dereva wa Gari aina Scania kwenda kuligonga Gari lilokuwa
limewabeka viongozi hao,ambapo gari hilo lilikuwa la nne kutoka gari
lililombeba Maalim Seif kwenye msafara huo.
إرسال تعليق