Raia wa Hong Kong wakivurumushiwa moshi
Makumi
kwa mamia ya waandamanaji wa Hong Kong wanaendelea na maandamano yao
kwa siku nyingine tena baada ya kudhoofisha maeneo muhimu ya jiji hilo
wakati wa mchana. Waandamanaji hao sasa wanamtaka Mkuu wa utawala wa
Hong Kong Leung Chun-Ying ajiuzulu..
Wakati huo huo Marekani
imesema inafuatilia kwa karibu kinachoendelea Hong Kong na imeutaka
utawala kuchukua hatua. Katika mkutano wa wanahabari msemaji wa Ikulu ya
Marekani Josh Earnest amesema Marekani inaunga mkono matakwa ya watu wa
Hong Kong.
"Duniani kote, na hii ni kweli katika Hong Kong na
maeneo mengine, Marekani inaunga mkono kimataifa, uhuru, kama vile uhuru
wa kukutana kwa amani na uhuru wa kujieleza. Marekani inautaka utawala
wa Hong Kong kuchukua hatua, na kwa upande wa waandamanaji kutoa maoni
yao kwa amani"

Post a Comment