Hospitali ya St. Harry Morogoro yafungwa.

Wizara ya afya na ustawi wa jamii  imeifungia hospitali  ya St Harry iliopo katikati ya mji wa Morogoro  kutokana na kutoa huduma za afya katika jengo ambalo halina viwango vya kutoa  huduma za matibabu   kwa wagonjwa  
Mganga mkuu  wa  mkoa wa morogoro dr  godfrey mtei   na mganga mkuu  wa manispaa  ya morogoro  Dr Abraham Mahizo ambao wameongoza zoezi  la kufunga hospitali hiyo wamesema wamefikiaumamuzi huo katika kutekeleza maagizo ya wizara ya afya  waliyoyatoa baada ya kufanya ukaguzi na kubaini kuwa hospitali hiyo haina vigezo vya kutoa huduma kwa wagonjwa  ingawa walipewa muda wa miezi kadhaa kuhamia katika jengo lao  jipya   lakini bado wamekiuka utaratibu na kuendelea kutoa huduma za afya katika hospitali hiyo.
Nae mmoja wa wasimamizi  wa hosipitali hiyo inamilikiwa na kanisa la international Karismatic church  of Tanzania  ICT, Mandia Kerem amesema wanasikitishwa na hatua ya wizara ya afya kufungia hospitali   hiyo kwani  kunamzunguzo yaliokuwa yakiendelea  na kwamba kufungwa huko  kutaathiri  na kusababisha usumbufu kwa wagonjwa wanaotegemea hospitali hiyo  kupata matibabu huku wakionekana kuwaelekeza wagonjwa  waliofika hospitalini hapo kuhamia katika  jengo lao jipya .

Post a Comment

أحدث أقدم