Ndugu zangu hawa watu wa shirika la Umeme wako wapi inafikia waya wa
umeme kupita juu ya paa la nyumba na kuwekewa tambara kuzuiya kuchunika,
hii ni hatari kwa wananchi wanaokaa katika nyumba hii huko kinuni siku
waya huo ukiwa tayari umeshachunika na kuleta madhara kwa wananchi wa
nyumba hii nani wa kulaumiwa ? ZECO au Mwananchi huyu . jioneeni wenyewe
na kutowa maamuzi ya jambo hili kazi kwenu wahusika. Kadhia hii imeiona
wakati nikiwa katika tembea yangu kinuni leo asubuhi.
إرسال تعليق