
Jeshi
la polisi mkoani Mtwara limefanikiwa kudhibiti maandamano ya chama cha
maendeleo na demokrasia Chadema kwa kufanya doria kila kona ya mji huo
huku wakiwa wamejiandaa kwa vifaa ili kupambana na yeyote atakayejaribu
kuvunja katazo la jeshi hilo la kuzuia maandamano mkoani humo.
Hata
hivyo ITV imeshuhudia jeshi hilo likiwa katika gari la polisi likipita
maeneo mbalimbali likiwemo eneo la Mkanaledi ambalo lilitajwa maandamao
ya Chadema yataanzia huko na hatimaye kuingia katikati ya mji.
Akizungumzia
ulinzi huo kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara Augustino Ulomi amesema
wamelazimika kutawanya askari kila kona sambamba na kuwaita viongozi wa
chama hicho kuwahoji baada ya kugoma kutii amri ya jeshi hilo ya kuzuia
maandamano na kuamua kusambaza vipeperushi vya kushawishi wananchi
kujitokeza katika maandamano kupinga kuendelea kwa bunge maalum la
katiba
Kwa
upande wake mwenyekiti wa chadema wilaya ya Mtwara Ibrahimu mandoa
amesema pamoja na jeshi la polisi kufanikiwa kudhibiti maandamano hayo
zipo njia mbadala za kufikisha ujumbe kwa umma na serikali.
Kwa upande wa wananchi wameonekana kutounga mkono maandamano hayo kwa madai waadhirika wakubwa ni wao.
CHANZO: ITV TANZANIA
إرسال تعليق