Baadhi
ya Kamati za Bunge Maalum la Katiba zimependekezwa kuwepo kwa Ibara
mpya inayohusu kuanzishwa kwa Tume za Huduma za Sekta, mbalimbali
ikiwemo ya Afya, Elimu , Walimu na nyinginezo ili kuweza kukabiliana
na matatizo yanayowakumba.
Kamati hizo zimependekeza suala hilo, katika sura ya 13 na 14 ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa.
Hayo yamebainika leo wakati wa uwasilishaji wa taarifa za Kamati Namba
Moja hadi Kamati Namba Kumi na Mbili za Bunge hilo kuhusu uhakiki wa
Rasimu hiyo uliofanyika kwenye kikao cha arobaini na tatu
kilichofanyika mjini Dodoma.
Taarifa
hizo,ambazo zimewasilishwa na baadhi ya wenyeviti wa Kamati hizo na
baadhi ya wajumbe kutoka 201 waliopewa ridhaa za kuwasilisha.
Baadhi ya Kamati za Bunge hilo,ambazo zimependekeza suala ni Kamati namba 5 na 6.
Akizungumzia
kuhusu suala hilo, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati Namba Sita ya
Bunge hilo, mjumbe wa Bunge hilo, Charles Mwaijage alisema Kamati yake
inapendekeza kuongeza Ibara mpya ya 208A mara baada ya Ibara ya 208
itakayosomeka kama ifuatavyo:
“Kwa
kuzingatia umuhimu wa sekta za huduma za jamii kwa wananchi, Bunge
litatunga sheria ya kuanzisha Tume za Huduma za Sekta hizo, kwa ajili ya
uendeshaji wa ufanisi zikiwemo za Elimu,Afya na nyingine kadri mahitaji
yatakavyojitokeza ,” alisema Mwaijage.
Kwa
upande wa Kamati Namba Tano ya Bunge Maalum la Katiba,mjumbe wa Bunge
hilo, Paul Makonda akitoa taarifa hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti alisema,
Kamati hiyo inapendekeza katika sura ya 14 kuongezwa kwa kifungu kipya
kitakachounda Tume ya Utumishi wa Walimu na kusomeka :
(1)Kutakuwa na Tume ya Utumishi wa Walimu itakayoshughulikia, mishahara, maslahi, ajira na masuala ya kinidhamu kwa walimu.
(2)Bunge
litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu muundo, majukumu mambo
mengine kuhusu utkelezaji wa Tume ya Utumishi wa Walimu.
Akizungumzia kuhusu suala hilo, Ezekiah Olouch, aliomba Kamati ya Uandishi ya Mhe. Andrew Chenge kuliangalia.
Alisema
zawadi ambayo watamkumbuka na walimu, Mwenyekiti wa Bunge hilo, Mhe.
Samuel Sitta na Bunge hilo kwa walimu hao ni kuingizwa kwa tume hiyo
ambayo itasaidia kutatua mattaizo ya walimu kwa asilimia 90.

إرسال تعليق