| HALIMA MDEE mwenyekiti wa BAWACHA akizungumza nna wanahabari Jijini Dar es salaam. |
Baraza la wanawake wa chama cha democrasia na maendeleo
chadema BAWACHA wamekuwa wa kwanza kuipinga rasimu ya tatu
iliyowasilishwa bungeni jana na kutangaza kuandamana hadi ikuliu ya jiji
la dar es salaam kupeleka kilio chao kwa kile walichoitwa kushindwa
kuwapa wanawake nafasi stahiki katika rasimu hiyo
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam mwenyekiti wa
baraza hilo BAWACHA ambaye pia ni mbunge wa kawe HALIMA MDEE amesema
kuwa kuwapa wanawake nafasi za uongozi za hamsini kwa hamsini kama
rasimu hiyo ilivyoelekeza bado sio kipaumbele cha wanawake wa Tanzania
ila kinachofanyika ni kuendelea kuwalaghai wanawake wa Tanzania.
Aidha amesema kuwa rasimu hiyo bado haimjali mtanzania kwani
kuna mambo mengi ambayo yameondolewa yalikuwepo kwenye rasimu ya
WARIOBA.
Wanawake hao wametangaza kufanya maandamano wiki moja ijayo
ambayo amekataa kutaja siku rasmi kwa kile alichokisema kuwa bado
wanafanya maandalizi ambapo yatakuwa ya amani ambapo amewataka polisi
kuwalinda kwani maandamano hayo yatakuwa ya amani na utulivu mkubwa
yakiwa na lengo la kupeleka ujumbe kwa watanzania wote juu ya mchakato
huo wa katiba.
إرسال تعليق