Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi katika kata ya
Mponde, akiwa katika ziara ya kukagua na kusimamia utekelezaji wa ilani
ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya
kuzitatua, katika jimbo la Bumbuli, wilayani Lushoto mkoani Tanga,
Septemba 29, 2014.
Akizungumza na mamia ya wananchi waliofurika kwenye viwanja vya
Kijiji cha Mponde, Kinana ameitaka serikali kuwachukulia hatua za
kisheria viongozi wote waliohusika kwa namna moja au nyingine
kusababisha kiwanda cha Chai cha Mponde, kufa baada ya kubinafsishwa kwa
njia zinazoashiria kutofuata utaratibu unaotakiwa.
Pia Kinana ameahidi kulifikisha suala hilo katika vikao vikubwa
ikiwemo cha Kamati Kuu ya CCM, ili kuhakikisha unapatikana ufumbuzi wa
kero hiyo ikiwemo kuwachukulia hatua viongozi waliohusika.

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi baada ya kuwasili
katika kijiji cha Mbuzii kushiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM kata ya
Mbuzii, katika jimbo la Bumbuli, wilayani Lushoto mkoa wa Tanga, leo
Septemba 29, 2014. Kushoto ni Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba.

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akijadili kwa makini jambo na Mbunge wa
Bumbuli, Waziri Januari Makamba, wakati wa kushiriki ujenzi wa Ofisi ya
CCM Kata ya Mbuzii, jimboni humo, leo, Septemba 29, 2014.

Mbunge
wa Bumbuli, Januari Makamba akizungumza wakati wa makaribisho ya katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akushiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM, Kata
ya Mbuzii jimboni humo mkoani Tanga, leo Septemba 29, 2014. pamoja naye
ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.

Katibu
wa NEC, Itikadi na uenezi, Nape Nnauye akizungumza wakati wa
makaribisho ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (Wapili kushoto),
kushiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Mbuzii, katika jimbo la
Bumbumuli, Lushoto mkoani Tanga leo Septemba 29, 2014. Watatu kushoto
ni Mbunge wa jimbo hilo, Januari Makamba.

Mbunge
wa Bumbuli, Januari Makamba (kulia) akimuonyesha Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana eneo la Ofisi ya CCM Kata ya Mbuzii, linalojengwa
pamoja na ukarabati wa ofisi ya zamani ya Chama ambayo ilikuwa imechakaa
kutokana na kuwa ya muda wa miaka mingi tangu enzi za Tanzania kupata
Uhuru

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki Ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata
ya Mbuzii, leo Septemba 29, 2014, akiwa katika ziara ya kukagua
utekelezaji wa ilani ya CCm na kukagua uhai wa Chama katika jimbo la
Bumbuli wilayani Lushoto mkoa wa Tanga. Kulia ni Mbunge wa jimbo hilo,
Januari Makamba akifanya 'kibarua' cha kumpa tofali Kinana..

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua jengo la zamani la Ofisi ya
CCM Kata ya Mbuzii ambalo linafanyiwa upanuzi na ukarabati, alipofika
kushiriki ujenzi wa Ofisi hiyo, leo katika jimbo la Bumbuli mkoani
Tanga. Nyuma yake ni Mbunge wa jimbo hilo, Januari Makamba

Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrah,man Kinana akisalimiana na Mzee aliyesema kwamba
amewahi kuwa dereva wa wakoloni, alipokutana na Kinana aliyewasili
kushiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Mbuzii, jimbo la Lushoto mkoa
wa Tanga.

Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimkabidhi fungua na hati za pikipiki,
kiongozi wa madereva wa Bodaboda katika kijiji cha Dule B, Kata ya
Mbuzii wilyani Lushoto mkoa wa Tanga. Pikipiki hiyo imetolewa na Mbunge
wa Bumbuli, January Makamba.

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwatazama Katibu wa NEC, Itikasi na
Uenezi, Nape Nnauye na Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba wakiendesha
pikipiki za waendesha bodaboda wa Kijiji cha Dule B, Kata ya Mbuzii,
katika jimbo hilo wilayani Lushoto mkoa wa Tanga.

Mkuu
wa Wilaya ya Lushoto, Majid Mganga akiendesha boda boda wakati msafara
ukienda kwenye uzinduzi wa shina la wajasiriamali la Maisha Plus kata ya
Dule.

Gari
la Maofisa wa CCM na Waandishi wa habai walioko kwenye msafara wa
katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana likiwa limevunjika kioo baada ya
gari hilo kukwaruzana na lingine, wakati msafara ulipowasili katika
Kijiji cha Dule B, kuzindua shina la wakereketwa wa CCM ambao ni
wajasriamali wa mradi wa kufyatua matofali wa Kikundi cha Maisha Plus.
Hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo.

Mbunge wa Jimbo la Bumbuli ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba
akiwasalimu wajasiriamali wa Maisha Plus wakati wa ziara ya Katibu mkuu
wa CCM, Abdulrahman Kinana .

Wakazi
wa kata ya Dule B wakisikiliza kwa makini hotuba za viongozi wao kabla
ya kuzinduliwa kwa shina la wajasiriamali la Maisha Plus.

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasalimu wajasiriamali wa Maisha
Plus ambapo alizindua shina la CCM wajasiriamali wa Maisha Plus katika
kata ya Dule B

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kupasua mawe kwenye kambi ya
Maisha Plus ,jimbo la Bumbuli wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kufyatua matofali .

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijiandaa kuukata muwa pamoja na
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Mheshimiwa January Makamba

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akila muwa, Maisha Plus

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimuelekeza Mbunge wa Jimbo la
Bumbuli January Makamba namna ya kupiga randa kwenye Kituo hicho cha
Maisha Plus.

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipandisha bendera ya CCM kuzindua
shina la wakereketwa Wajasriamali wa CCM Kikundi cha Maisha Plus, eneo
la Dule B ,jimbo la Bumbuli wilaya ya Lushoto.

Maisha Plus Bumbuli.

Abdulkarim
Jambia aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema kata ya Vuga akionyesha juu kadi
yake ya CCM baada ya kurejea rasmi CCM kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika Mponde.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijionea namna mashamba ya chai
yalivyogeuka vichaka . Katibu Mkuu ameongozana na Mbunge wa Jimbo la
Bumbuli Mheshimiwa January Makamba.

Mamia
ya wananchi wakiwa wamefurika kwenye mkutano wa hadhara aliohutubia
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, katika Kata ya Mponde, jimbo la
Bumbuli wilayani Lushoto mkoani Tanga, leo Septemba 29, 2014.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia kwenye mkutano huo wa Kinana

Baadhi
ya watu wakiwa wamekaa ,kilimani kuhakikisha wanamuona Katibu Mkuu wa
CCM, Abdulrahman Kinana akipohutubia Mkutano wa hadhara katika Kata ya
Mponde kwenye jimbo la Bumbuli mkoani Tanga leo.

Mbunge
wa Bumbuli Januari Makamba akieleza kero kuhusu zao la chai na kufa kwa
kiwanda cha Chai cha Mponde, alipokaribishwa na Katibu Mkuu wa CCM
Abdulrahman Kinana akuzungumza na wapigakura wake.

Mwananchi
wa Mponde akieleza kwa hisia, jinsi wananchi wa Bumbuli
wanavyosumbuliwa na kero ya kufa kiwanda cha Chai kilichopo Kata ya
Mponde kwa miaka mingi sasa. Asilimia kubwa ya wakazi wa Bumbuli ni
wakulima wa Chai.
إرسال تعليق