Meneja mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bwana Innocent Mungy akisisitiza jambo.
Na Benedict Liwenga, Maelezo-DSM.
Mitandao
ya kijamii ni mizuri katika kuhabarisha umma endapo inatumiwa kulingana
na madhumuni iliyotengenezwa, kwani ina nguvu ya kusambaza habari kwa
haraka na kwa wakati hapa duniani.
Pamoja
na umuhimu nwa mitandao hii ya kijamii, kuna baadhi ya watu ambao wao
hujiona kuwa wameendelea katika ulimwengu wa kisayansi na teknolojia
kiasi cha kuanza kuitumia mitandao hiyo kinyume na malengo kwa kutumia
kuiba taarifa mbalimbali za watu na hata usalama wa maeneo muhimu
ikiwemo benki, ofisini, mashuleni na sehemu kadha wa kadha.
Watu
hawa kwa jina la kisayansi na teknolojia hujulikana kama ‘Hackers’ au
Wezi wa mitandao kwa kisawahili, na wamekuwa wakivumbua mbinu mbalimbali
kila kukicha ili kuweza kutimiza adhma yao ya kuingilia mitandao mingi
iliyopo duniani na wakati mwimngine wamekuwa wakitumika katika shughuli
za kigaidi ulimwenguni.
Kwa
mujibu wa taarifa mbalimbali toka mitandaoni, kuna mbinu nyingi
zitumiwazo na hackers hawa katika kuiba taarifa mbalimbali kutoka kwenye
takirishi (Computer) hata simu za mkononi kwa njia ya mtandao (internet) na njia hizi huwa zimekuwa zikiboreshwa kila kukicha.
Wezi wa mitandao wengi wamekuwa wakitumia visaidizi vya kompyuta (softwares) zijulikanazo kama Keyloggers
ambazo ni hatari sana katika kuiba taarifa toka sehemu yoyote endapo tu
mmiliki wa kompyuta ataiacha kompyuta yake kutumiwa na watu
wasiofahamika ama katika ofisi mtu mharibifu ataingia na kuingiza katika
mfumo wa kuongozea kompyuta kisaidizi kama hiko, kutokana na hilo
software hizo hukusanya taarifa za mtu pasipo mtumiaji kujua
kinachoendelea na taarifa hizo hutumwa kwa njia ya barua pepe kwenda kwa
mharifu ambaye yeye anakuwa anazipata kadri atakavyo juu ya chochote
akifanyacho mtu, na moja ya sifa za software hizo ni kwamba hazionekani
ndani ya mfumo wa kuongozea kompyuta kirahisi.
Mbinu nyingine watumiazo watu hao ni kwa njia ijulikanayo kwa kimombo kama ‘Phising’
ambapo ukurasa unaofanana sawia na ukurasa halisi wa website
hutengenezwa kwa madhumuni thabiti ya kuiba nenosiri ama taarifa zozote
kuhusiana na kitu chochote, njia hii ni hatari pia ingawa haina tofauti
sana na njia ile ya key logging kwani katika njia hii kazi kubwa inayofanyika ni kuweko kwa kurasa feki ambayo inayofanana na kurasa halisi ya website fulani.
Ili
tuweze kujikinga na matukio haya ya wizi wa taarifa kwa njia ya mtandao
kuna mambo muhimu ya kuzingatia ambayo tunapaswa kuwanayo makini wakati
wote tunapozitumia kompyuta zetu.
Kwaza
kabiasa, ili tuweze kujiepusha na njia itumiwayo na hackers ijulikanayo
kama Key-logging ni vema kuepuka kuazimisha kompyuta zetu kwa watu
tusiowajua ama kutumia mbinu ya kubofya kitufe cha Ctrl + shift + Alt + K
vyote kwa pamoja ili kuweza kujua uwepo wa kisaidizi kama hiko katika
kompyuta na kama ikitokea kimekuja kisanduku kinachokudai kuweka
nenosiri basi ujue hapo kuna mtu anachunguza taarifa zako katika
kompyuta yako pasipo wewe kujua, hivyo chukua tahadhari kwa kumtafuta
mtaalam aweze kuondoa kisaidizi hiko.
Pia yatupasa kuhakikisha kuwa Windows Firewalls zilizopo ndani ya mifumo ya kuongozea kompyuta zetu ziko wazi wakati wote kwani firewall
inasaidia kulinda takirishi yako dhidi ya wezi wa mitandao (hackers)
ambao wanaweza kujaribu kuiharibu kwa lengo la kutaka kupata taarifa
zilizomo ndani, kufuta taarifa, na hata kuiba baadhi ya neno siri za
baadhi ya taarifa zako.
Ili kujikinga na wizi wa taarifa zetu katika kompoyuta zetu, tunapaswa kuzingataia kuingiza ama ku-update Vizuizi virusi (Antivirus)
mara kwa mara kwani vizuizi hivyo vimetengenezwa kwa ajili ya kuzuia
virusi ama visaidizi kompyuta chokozi ili zisiweze kuiingia ndani ya
mfumo wa kompyuta na endapo ikitokea imegundua kirusi cha namna yoyote
ile, basi inafanya kazi ya kukiondoa ama kukifanya kisiweze kudhuru
kompyuta wakati wote.
Bila
shaka lolote, Virusi vinaweza kuharibu mfumo wa kuongozea kompyuta
pasipo mtumiaji mwenyewe kujua licha ya baadhi ya vizuizi virusi kuwa na
tabia ya kuji-update vyenyewe.
Kuweka ama ku-update Antispyware Technology ni jambo linghne la usalam dhidi ya hackers kwani Baadhi ya spyware huwa na tabia ya kukusanya taarifa za mtu pasipo ridhaa yake kama ilivyo kwenye key-logging na Phising
au huwa na tabia yakuweka matangazo yasiyo na ulazima katika kurasa
Fulani iliyopo katika mtandao wa kompyuta, sasa hii ni hatari kwa
usalama wa taarifa za mtu kwani hutumika pia kukwapua, hivyo hatunabudi
kuwa makini na baadhi ya matangazo yenye kututaka kupakua visaidizi
fulani pasipo malipo kwani mara nyingi huwa ni feki na wakati mwingine
huwa na virusi vyenye kuweza kutumika kuiba taarifa ndani ya takirishi
yako.
Katika
hali yoyote ile ni vema kwa watumaiji wa mitandao ya kijamii kuepuka
kutunza nenosiri katika kompyuta zao kwa lengo la kuondoa usumbufu
wakati wanapotaka kuingia tena katika kurasa zao kwani njia hiyo nayo ni
hatari kwasababu mtu anapoacha nenosiri lake liko (logged in) au unaposema (remember me next time) unatengeneza njia rahisi kwa hacker kujua nenosiri lako kwa kufanya kitendo kijulikanacho kama (Inspect elements Q) yaani zile doti zinazowakilisha neno siri lako (******).
Katiko hilo, mharifu anachokifanya hapo ni kuhailaiti hizo doti (nyota) kisha anabofya katika kipanya upande wa kulia (right clicking) kisha anaenda mwisho katika sehemu iloandikwa (inspect elements Q) kisha anafanya uhariri (editing) katika kipengele kilichokuwa hailaitedi kwa rangi ya bluu kilichoandikwa neno ‘passoword’, hapo anafuta na kuandika neno ‘TEXT’ kisha anabofya kitufe cha ‘Enter’
na akishamaliza kufanya hivyo nenosiri lenyewe linajibadilisha kwenda
mfumo wa maneno badala ya doti kama ilivyokuwa hapo mwanzo, hivyo
humuwezesha kujua tarakimu za nenosiri la akaunti yako ya mtandao wa
kijamii uliocha wazi.
Njia
nyingine ya jinsi ya kujikinga na wizi wa kimtandao, tunahitaji kuwa
makini na vitu tunavyopakuwa toka mitandaoni hasa vibebaji (attachments)
toka kwa watu tusiowafahamu au wakati mwingine kwa watu tunaowajua
kwani hata hao hutumika katika kusaidia kuibwa kwa taarifa zetu kwa
malengo yao binafsi.
Pia
ni vema kuepuka kukubali marafiki tusiowajua katika mitandao mingi ya
kijamii ikiwemo facebook, twitter, Whatsapp, na mingineyo kwani baadhi
ya hackers wanatumia majina yasiyosahihi (fake names) kuomba urafiki kisha hutumia mwanya huo pia katika kuiba taarifa zetu kiurahisi.
Kwa
upande wa mabenki, ni vema kuachana na mifumo ya kizamani ya kuongozea
kompyuta iliyounganishwa na Mashine za kutolea fedha maarufu kama (ATM)
au Automatic Teller Machine kwa kimombo, kwani hiyo ni hatarishi
kwasababu mifumo ya kizamani, mfano Microsoft Windows XP ni
mifumo ilikwishapitwa na wakati na hata Kampuni yenyewe ya Microsoft
imewataka watumiaji kuwa makini nayo kwani haina-updates tena hali
inayopelekea kuwa katika hatari ya kuvamiwa na wezi wa mitandao kwa
kutumia software za kisasa zenye uwezo wa hali ya juu katika kuiba
taarifa.
Katika matumizi ya kadi zetu za kutolea fedha benki (ATM Cards)
tunapaswa kuwa makini kuepuka kushea namba za siri kwa marafiki au
wapenzi na tujitahidi kuacha tabia ya kutumia nenosiri la kadi hizo kama
nenosiri katika akaunti za mitandao ya kijamii kwani hackers nao
wamekuwa watu wazuri wa kubashiri taarifa pindi wanapomlenga mtu.
Ili
kujiweka salama dhidi ya wezi wa mitandao, basi tujitahidi kutoa
taarifa zozote za kiusalama kwa vyombo vya usalama yaani Polisi au
kupeleka malalamiko kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) pindi
tunapoona taarifa za uvunjwaji wa sheria za matumizi ya mitandao, mfano
mtu akiona kuna hitilafu katika taarifa za muamala wa fedha zake katika
akaunti yake ya benki fulani basi atoe taarifa kwa benki husika ili wao
waweze kutafuta tatizo na kutoa ufumbuzi.
Pamoja
na haya yote Watanzania wamehimizwa kuacha matumizi mabaya ya mitandao
ya jamii ikiwemo kuweka picha za utupu, kusababisha ugomvi, kuwahimiza
wengine kwa mambo yasiyo ya kweli, kupotosha jamii na kuvuruga
maendeleo.
Akitoa
rai hiyo Meneja mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),
Bwana Innocent Mungy alisema kuwa kuna ongezeko la matumizi ya intanenti
kwa watanzania hasa mitandao ya kijamii ambayo ni facebook, twiter,
Instagram, BBM, LinkedIn na Blogs mbalimbali kwa mambo yasiyofaa na
kuleta athari kwa jamii.
Alisema
matukio yanayofanyika katika mitandao hiyo na kuleta athari ni utapeli,
kulipiza kisasi na ugomvi unaoanzia mitandaoni na kuendelea hadi kwenye
uhalisia.
“Kuna
utapeli wa kutumia huduma za mawasiliano na ugomvi wa makundi
yakugombana kupitia mitandao kwa majina kama timu fulani na timu fulani
inayosababisha kuvunjika kwa amani na kusababisha matusi pande zote,”
alisema Mungy.
Mungy
aliongeza kuwa ni kosa la jinai kutumia mawasiliano vibaya kama
ilivyoainishwa katika sheria ya mawasiliano ya Kielektroniki na Posta
(EPOCA) ya mwaka 2010 na kutaka mawasiliano yatumike vizuri kudumisha
amani ya Tanzania.
“Mamlaka
inapenda kuukumbusha umma kuwa ni kosa la jinai kuuza laini ya simu
iwapo siyo wakala au mtoa huduma, kutumia simu isiyosajiliwa, kutumia
njia yeyote ya mawasiliano kuvuruga amani na kumsaidia mtu mwingine
atende kosa,” alisema.
Kwa
mujibu wa Mungy ni kosa la jinai kuweka picha za marehemu, mtoto na
zinazoonesha utupu katika mitandao ya kijamii huku akibainisha kwamba
faini ya kosa hilo ni shilingi za Kitanzania 750,000 na kifungo cha
miezi mitatu gerezani.
Kutokana
na haya, lazima tutambue kuwa mitandao ya kijamii si dhambi wala si
vibaya kuitumia, kwani haijatengenezwa kwa madhumuni ya kumkomoa fulani
ama kwa lengo la kuelimisha watu juu ya namna ya kuiba taarifa za watu
wengine, bali inetengenezwa ka madhumuni ya kuwakutanisha watu wa sehemu
mbalimbali duniani kuweza kuhabarishana juu ya mambo mbalimbali
japokuwa baadhi ya watu hao wamekuwa wakiitumia vibaya kinyume na
maelngo ya uwepo wake.

إرسال تعليق