
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Furahisha Kirumba, mjini Mwanza.

Sehemu ya umati uliohudhuria kwenye Mkutano wa hadhara wakimsikiliza katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Furahisha Kirumba, mjini Mwanza.
Na Khamis Haji, OMKR
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF,
Mhe. Maalim Seif Sharifa Hamad amesema migogoro inayowakumba wakulima na
wafugaji na kusababisha mauaji inasababishwa na Serikali iliyopo chini
ya Chama cha Mapinduzi kukosa sera sahihi ya Kilimo na Ufugaji.
Maalim Seif ameyasema hayo katika mikutano tafauti akiwa katika ziara ya siku nne mkoani Mwanza kwa ajili ya kuzindua miradi ya maendeleo iliyo chini ya Kata zinazoongozwa na CUF pamoja na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara.
Akizungumza na wananchi baada ya
kuzindua daraja katika Kata ya Igogo amesema inasikitisha kuona kila
siku wakulima na wafugaji wakiuana kwa kugombea maeneo ya kilimo na
kulishia mifugo huku Serikali ikishindwa kudhibiti hali hiyo.
Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema kusingekuwa na mauaji kati ya
wakulima na wafugaji iwapo Serikali ingekuwa na Sera thabiti inayoanisha
maeneo maaluma kwa ajili ya ufugaji na maeneo maalum ambayo ni kwa
shughuli za kilimo pekee.
“Kama Serikali ingekuwa na Sera
inayoanisha haya ni maeneo ya ufugaji na haya ni ya kilimo
tusingeshuhudia mapigano na mauaji haya, wakulima na wafugaji wangefanya
kazi zao kwa utulivu na kazi zao zingewapatia maslahi makubwa”, amesema
Maalim Seif.
Amesema Tanzania imejaliwa maliasili
nyingi kuliko nchi nyingi duniani na iwapo tungeweza kuzitumia vizuri
hakuna sababu nchi hii kuwa miongoni mwa nchi masikini.
Maalim Seif ameeleza kuwa mbali na
maliasili zilizopo chini ya ardhi kama vile madini, gesi na mafuta,
Tanzania imejaaliwa kuwa na hali ya hewa inayotafautina katika maeneo
ambayo inaifanya nchi kuzalisha mazao tafauti tafauti.
Hata hivyo, amesema kukosekana kwa sera
muafaka kuna sababisha wananchi walio wengi kushindwa kunufaika na neema
hiyo na kutoa mfano, licha ya wananchi wa kanda ya Ziwa kuongoza kwa
kilimo cha Pamba, lakini hakuna hata kiwanda cha nguo.
“Wananchi wa Kanda hii nyinyi ndio
mnaozalisha Pamba, lakini pamba hiyo inasafirishwa Ulaya, wanatengeza
nguo wanavaa na baadaye wanatuletea sisi ikiwa ni mitumba na sisi
tunaivaa”, alieleza Maalim Seif.
Akihutubia katika mkutano wa hadhara
katika uwanja wa Furahisha Kirumba, Maalim Seif amesema wananchi hawana
budi kujiandaa kufanya mageuzi ya uongozi wa nchi kwa kuwaweka
madarakani viongozi wenye uwezo na mtazamo mpya wa kuleta maendeleo ya
wananchi.
Naye Mbunge wa Nyamagana kupitia
CHADEMA, Ezekiel Wenje akihutubia katika mkutano huo amesema njia
muafaka ya kuleta mageuzi ya kiuongozi nchini ni vyama vya upinzani
kuendeleza ushirikiano na kuwa na mgombea mmoja katika ngazi zote.
Wenje amesema yeye binafsi yuko tayari
kufadhili safari ya viongozi wakuu wa CHADEMA, CUF na NCCR Mageuzi
wakajifungie nchini Sychelles ili waweze kupata mgombea mmoja ambaye
watamsimaisha kuwania Urais katika uchaguzi mkuu wa mwakani kupitia
Ukawa.
Hata hivyo, akilifafanua hilo, Maalim
Seif amesema jambo hilo wala halihitaji kwenda kuamuliwa nje ya nchi, na
badala yake viongozi hao wanaweza kutoa maamuzi hayo hapa hapa nchini.
إرسال تعليق