Madiwani
wa wa Halmashauri ya Mpanda wakiwa katika Picha ya Pamoja nje ya ofisi
ya hifadhi ya wanyama pori katavi kabla ya kuanza safari ya kutembelea
hifadhi hiyo.

Hapo
wanyama aina ya viboko wakionekana kuhangaika kutokana na ukosefu wa
maji ya kutosha kwenye Mto Ikuu na kavuu ambayo inaitwa Shule ya Viboko
na Mamba,
Huyo ni mnyama mfalme wa pori simaba akiwa amejipumzisha kivulini huku akiwa katika mawindo yake kama ilivyo kawaida yake.
Hao ni viboko wakilandalanda nje yam to Ikuu ambao umekauka maji na wengine wakiwa majini kama wanavyoonekana hapo
Mnyama
aina ya Tembo wakiwa kwa mbali wakikimbia kutafuta maji ili kuweza
kupoza koo zao baada kupata lishe na kwa nyuma watoto wa Tembo
wakifuata.
Mnyama
aina ya Tembo wakiwa kwa mbali wakikimbia kutafuta maji ili kuweza
kupoza koo zao baada kupata lishe na kwa nyuma watoto wa Tembo
wakifuata.
Madiwani wa Halamshauri ya Wilaya
ya Mpanda watembelea Hifadhi ya Taifa ya Katavi na kujionea wenyewe
athari ya uharibifu wa mazingira unavyoathiri wanyama katika mbuga ya
katavi hasa wanyama aina ya Viboko na mamba kutoka na ukame unaikabiri
mbuga hiyo kupelekea wanyama hao kwenye mto Ikuu Katavi na ziwa Chanda
kukauka na kuwafanya wanyama hao kufa kutokana na ukosefu wa maji.
Madiwani wapatao 13 wakiongozwa na
Mwenyekiti wa Halmashauri wakifuatana na watalaam kutoka Idara ya
Maliasili na Mazingira,Kilimo, na Idara ya Utumishi na Utawala walifanya
safari kutembelea mbuga hiyo na kujionea hali ilivyo katika hifadhi
hiyo ambapo walifika eneo linaloitwa mto ikuu unaopokea maji kutoka mto
Katuma ambao ndi tegemeo kuu la kupeleka maji kwenye mbuga hiyo ukiwa
umekauka kutokana na uharibifu mkubwa unaofanywa na wananchi kwenye
vyanzo vya mto huo.
Maeneo yaliyoathiriwa sana na
ukame ni eneo la Mto Ikuu ,Kuu,na Chanda ambapo makundi ya wanayam aina
ya viboko walikuwa na hali mbaya wakihangaika kutafuta maji huku
wengine wakiwawamelala hoi bin taabani .
Mbali ya wanyama aina ya Viboko
ambao ni wengi katika mbuga hiyo pia wanyama Mamba ,makundi ya
Tembo,Nyati,Twiga, Pundamilia,na wengineo pamoja na makundi ya ndege
walikuwa wamekusanyika kwa pamoja huku yakipigania maji kidogo
yaliyosalia katika vidimbwi vya mto huo angalau waweze kutuliza kitu
waliyokuwanayo dhahiri shahiri wanyama katika hifadhi ya Katavi wanahali
mbaya.
Hifadhi hiyo ambayo ni kubwa nay a
tatu kwa ukubwa hapa nchini ni rasilimali pekee na hazina kubwa kwa
taifa kutokana na wanyama waliomo,wakubwa wakubwa kama nyati, tembo
Simba ,kongoni viboko ,makundi ya ndege na mimea ya aina mbali mali
amabyo ni kivutio kikubwa kwa watalii lakini inakabiliwa na uharibifu
mkubwa kutokana na kukoasa maji kwa wanyama hao kwa kile kilichoelezwa
uharibifu wa mazingira unaofanywa na wananchi kwenye vyanzo vya maji vya
mto katuma ambao unapeleka maji kwenye mbuga hiyo.
Akizungumzia hali ya uharibifu
unaofanyika wa mazingira katika hifadhi ya Katavi Mhifadhi wa ujirani
mwema katika hifadhi ya Taifa ya Katavi David Kadomo ameelaz kuwa
Hifadhi ya Taifa ya Katavi inakabiliwa na changamoto ya ujangili mkubwa
hasa wa kuuwawa kwa Tembo,na upo wasiwasi mkubwa kuwa huenda Tembo hao
wakatoweka kutokana na ujagili unaofanyika katika hifadhi hjiyo.
Mbali ya ujagili pia hifadhi
inakabiliwa na changamoto ya wafugaji kuingiza mifugo ya kwenye hifadhi
hiyo ya Taifa ya Katavi na kufanya mahali pa malisho, wapo wafugaji
wengi wanavamia hifadhi na makundi yao ya ngombe katika hifadhi hiyo
pamoja na juhudi zinazofanyika kuilinda bado watu wanaingia na mifugo
yao.
Mhifadhi Kadomo akaeleza kuwa pia
maeneo yaliyohifadhiwa ambayo hayako kwenye hifadhi amabayo ni maeneo ya
uhifadhi wa wanyapori ambayo yako mita miatano kutoka eneo la hifadhi
na kijiji ya WMA ya Ubende na Mpimbwe yanaonekana kuvamiwa na kufanywa
shughuli za kibinadamu za kilimo,mifugo na makazi ya watu jambo ambalo
siyo taratibu kwa kuwa hayaruhusiwi kufanywa kwa shghuli hizo za
kibinadamuzinazoathiri mazingira.
Kwa kuwa sheria ya uhifadhi wa
wanyama pori imeeleza wazi kuwa mita 500 zilizotengwa kutoka nje ya
hifadhi shughuli zinazofanyika hapo zisiwe zile zinazoweza kuathiri
mazingira lakini maeneo mengi kwenye hifadhi hizo za wanyama
yanaharibiwa na viongozi wanaona wapo.
Wananchi wanagawiwa mashamba
katika maeneo hayo na viongozi wanaangali akaawaomba madiwani kwa kuwa
wako karibu na wananchi wawaelimisha juu ya kutoharibu mazingira na
umhimu wa uhifadhi ili wasiendelee kuharibu mazingira katika hifadhi
hizo na ile ya Katavi.
Pia alielezea changamoto ya
uchomaji moto mapori na hata maeneo yaliyojirani na hifadhi ,vilevile
utupaji taka hovyo ndani ya hifadhi pamoja na mwendo kasi wa magari
yanayopita katika hifadhi hiyo kwa kuwa hifadhi inapitiwa na barabara
mbili ziendazo sumbawanga na ile ya Tabora wanyama wanagongwa sana
akashauri madereva wanaotumia mbarabara hizo wajitahidi kuzingatia
sheria na kupunguza mwendo waende mwendo wa kawaida ili kuepuka
kuwagonga wanyama katika hifadhi hiyo.
Kwa UPANDE WAKE Diwani wa Kata ya
Kabungu Selemani Kasonso alieleza kuwa watajitahidi kutoa elimu kwa
jamii kuhakikisha wanaokoa maisha ya wanyama hao ambao wanategemea maji
yam to katuma na kwenye kata yake wapo watu wanaoharibu mazingira yam to
huo kwa kuweka vikingamaji ili maji yasiweze kupita kwa ajili ya kilimo
cha mpunga akasema watalipigia kelele kwelikweli kwenye vikao vyao
mpaka wafanikishe,.
Akaongeza kuwa wanyama hao
wanateseka sana na wanakufa haiwezekani rasilimali kama hii ipotee hivi
kizazi kijacho kitakuja kutuhumu kwa kushindwa kutunza wanyama hao na
kuhifadhi mazingira ili waendelee kuwepo milele na milele,akasema mfano
wazungu waliwauwa wanyama wote kule kwao na kuharibu mazingira hatimaye
wakatoweka sasa ndiyo maana unao wanakimbili huku kwetu hasa Tanzani
kuja kuaangalia kwa kuwa hkule kwao hawapo tena,ni wajibu wetu sasa
kuhakikisha tunalisimamia hili.alisema Kasonso.

إرسال تعليق