
Kwa mujibu
wa takwimu za Shirika la Afya Duniani, WHO zilizotolewa mwaka 2011, Vifo
vilivyotokana na magojwa ya moyo nchini Tanzania vilifikia idadi ya
watu 19,083, au asilimia 4.33% ya idadi ya vifo vyote. Na takwimu hizo
zilionyesha idadi ya wanaofariki ni watu 117.64 kati ya watu 100,000, na
takwimu hizi zikiiweka Tanzania katika nafasi ya 87 ulimwenguni.
Magonjwa
haya ya moyo yanasababisha vifo vipatavyo idadi ya watu milioni 12 kwa
mwaka duniani kote. Hata hivyo shirika la Afya Duniani limekua likifanya
jitihada za lazima za kujaribu kupunguza vifo vitokanavyo na magonjwa
ya moyo na sababu zinazochangia kuongezeka kwa vifo hivyo.
Magojwa
haya ni pamoja na ugonjwa wa moyo, kiharusi, shinikizo la damu , ugonjwa
wa pembeni wa mishipa ya moyo, , ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa na moyo
kushindwa kufanya kazi ipasavyo. Katika kuonyesha kukua kwa maendeleo
ya kiteknolojia ya huduma za afya, Hospitali ya Apollo ya mjini
Gujarat , katika mji wa Ahmedabad, ilifanikiwa kufanya upasuaji
unaojulikana kitaalam kama ‘Bentall Surgery’ kwa mwanamke aliyekuwa na
zaidi ya miaka 50. Upasuaji wa aina hii mara nyingi ni adimu kufanyika
katika nchi ambazo ni masikini na zenye wataalamu wachache, ama zenye
mfumo wa chini wa huduma za afya. Upasuaji huu uliofanywa kwa mwanamama
kutoka Tanzania, uliukuwa ni wa aina yake, na ulichukua muda wa saa
saba. Hii inaonyesha jinsi gani hospitali hizi zilivyo na uwezo na
utaalam wa hali ya juu.
Mama huyo
alikuwa akilalamika toka maka 2009 kuhusu maumivu ya mgongo, na
alipofanyiwa uchunguzi wa kina, ilionekana kuwa alikua na matatizo
katika moyo wake, ambayo hata hivyo hayangeweza kutibiwa hapa nchini.
Alipelekwa katika hospitali ya Apollo ya mjini Ahmedabad, hospitali
inayosifika kwa kufanya upasuaji kwa ufasaha na uhakika zaidi.
Mama huyu
alifanikiwa kufanyiwa upasuaji huo mgumu wa moyo uliochukua zaidi ya
masaa saba, ilionekana kuwa alikua na matatizo makubwa katika mishipa ya
Aorta ambayo yalisababisha moyo wake ushindwe kufanya kazi kama
kawaida. Hatimaye upasuaji huo ulifanikiwa, na pengine asingeweza kupona
kama bado angelikuwapo nchini hapa, na hali yake inaendelea vizuri.
“
katika masuala ya afya, bara la Afrika liko kama bara la Asia miaka 25
ama 30 iliyopita. Wale tu wenye kipato cha juu ndiyo wanaoweza kumudu
huduma za uhakika nje ya nchi’’, Anasema Dr Hari Prasad, mkurugenzi mtendaji wa hospitali za Apollo.
“Ni
wakati muafaka sasa wa kutumia uwezo wetu na utaalam wetu kuwatibu
wenye matatizo. Tulichoifanyia india hatuna budi kuifanyia dunia na nchi
zinazoendelea, Anaongezea Dr Pratap C Reddy, mwenyekiti wa hospitali wa za Apollo
Mbali na
Tanzania, Hospitali ya Apollo imepania kukita mizizi yake katika nchi
mbalimbali za Afrika , ambako imekua ikipokea idadi ya wagonjwa wengi
kutoka bara hili, na ina matarajio ya kuanzisha vituo kadhaa vya Afya
katika eneo la Afrika ya Mashariki na Afrika magharibi hapo mbeleni.
إرسال تعليق