
MAHAKAMA
Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam jana imetupilia mbali maombi ya
pingamizi la awali la kusimamisha Bunge la Katiba linaloendelea mjini
Dodoma, iliyofunguliwa na Mwandishi wa Habari Said Kubenea, kwa kuwa
wametumia kifungu cha sheria kisicho sahihi.
Kadhalika,
mahakama hiyo imetupilia mbali pingamizi hilo la awali, kwa kuwa
mlalamikaji ametumia kifungu cha sheria namba 2 kidogo cha (2) (JALA)
ambacho hakina mamlaka ya kufungua maombi hayo mahakamani.
Uamuzi
huo ulitolewa chini ya jopo lililoketi la majaji watatu, wakiongozwa na
Mwenyekiti Mh.Jaji Augustino Mwarija, Dr. Fauz Twaib na Aloyisius
Mujuluzi.
Jopo hilo lilisema mahakama imetupilia mbali pingamizi hilo la awali kwa sababu halina mashiko ya kisheria.
Upande wa mlalamikiwa uliongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Gabriel Malata na mlalamikaji Peter Kibatala.
Awali,
Mwanasehria Mkuu (AG) kupitia Naibu Mwanasheria Mkuu, George Masaju
kuiomba mahakama hiyo kutupilia mbali pingamizi hilo kwa kuwa maombi
yake ni batili kisheria na hayawezi kuthibitishwa mahakamani, hivyo
yatupiliwe mbali.
Katika
pingamizi hilo lililoambatana na hati ya kiapo, AG kupitia naibu wake,
amedai kuwa maombi hayo ya mlalamikaji yana dosari ambayo haiwezi
kurekebishika kwa kuwa zinahitaji kifungu maalum cha sheria kinachoipa
nguvu mahakama ya kuridhia maombi hayo.
Mapema
mahakamani hapo, Kubenea aliwasilisha maombi ya pingamizi la awali ya
kusimamisha Bunge hilo kwa muda yaliyopewa usajili wa namba 29 ya mwaka
2014, pamoja na maombi ya msingi ya tafsiri ya mamlaka ya Bunge yote
yalifunguliwa mahakamani hapo jana chini ya Hati ya Dharura.
Katika
kesi ya msingi iliyopewa usajili namba 28 ya mwaka 2014, Kubenea
anaiomba mahakama hiyo itoe tafsiri sahihi ya Mamlaka ya Bunge la Katiba
chini ya vifungu vya 25 (1) na 25 (2) vya Sheria ya Marekebisho ya
Katiba namba Namba 83 ya mwaka 2011.
Pamoja
na mambo mengine katika kesi hiyo ya kuomba tafsiri ya mamlaka ya Bunge
hilo, pia Kubenea amewasilisha maombi mahakamani hapo akiiomba
mahakama itoe zuio la muda la kusimamisha Bunge hilo ili kusubiri uamuzi
wa maombi ya tafsiri hiyo.
إرسال تعليق