Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, SACP, Geofrey Kamwela.
Na Nathaniel Limu, Singida
WATU
wawili mkoani Singida wamefariki dunia katika matukio tofauti, likiwemo
la Mwalimu wa shule ya msingi Kigogo jijini Dar-es-salaam, Hawa Idd
(34) baada ya kuchomwa kisu sehemu mbalimbali za mwili wake na mdogo
wake Ramadhan Iddi (24) anayedaiwa kuwa na matatizo ya akili.
Kamanda
wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, SACP, Geofrey Kamwela alisema tukio
hilo limetokea Septemba 23 mwaka huu saa 9.30 alasiri huko katika
hospitali ya mkoa mjini Singida.
Alisema
Septemba 22 mwaka huu saa 5.30 asubuhi kijana Ramadhan ilidaiwa
alitoka nyumbani kwao kwa mazingira ya kutatanisha na ndipo mwalimu Hawa
ambaye alikuja kwa ajili ya kushughulikia matatizo ya mdogo wake
huyo,walianza msako wa kumtafuta katika maeneo mbalimbali mjini Singida.
“Baada
ya kumtafuta katika mitaa mbalimbali hapa mjini na kumkosa, Hawa
alirejea nyumbani kwao Kibaoni na kumkuta mdogo wake Ramadhan,ameisha
rejea nyumbani. Haikuchukua muda wanandugu hao walianza kulumbana
kitendo kilichosababisha Ramadhan kuchomoa kisu kutoka kwenye mfuko wake
wa suruali na kumchoma dada yake tumboni, kichwani na kwenye mkono wa
kushoto”, alisema Kamwela.
Kamanda
huyo alisema Hawa aliweza kupiga yowe na majirani walifika mara moja na
kumkimbiza hospitali ya mkoa ambako alifariki dunia kesho yake alasiri
wakati akiendelea na matibabu.
Katika
tukio jingine, Kamwela alisema Mchiwa Jeremia (22) mkazi wa kijiji cha
Ipanduka tarafa ya Konko wilaya ya Manyoni, amefariki dunia Septemba 22
mwaka huu saa moja asubuhi baada ya kushambuliwa na wananchi wenye
hasira kali akidaiwa kuiba shilingi 115,000.
Alisema
Septemba 21 mwaka huu saa tisa alasiri Mchiwa anadaiwa kuvunja nyumba
ya Lukeresha Mdashi na kuiba kiasi hicho cha fedha.
“Kwa
sasa tunamshikilia Lukeresha kwa mahojioano zaidi na pindi
yatakapomalizika,mtuhumiwa tunatarajia kumfikisha mahakamani”,alisema.

إرسال تعليق