Mwimbaji wa Serebuka, Mwasiti ni mmoja kati ya wasanii wa
kike ambao hawaonekani sana kwenye shows za uwanjani lakini mwenyewe
anasema kuna shows zake zinazomuingizia pesa nyingi zaidi.
“Nafikiri watu wengi hawanionagi kwenye shows za uwanjani sana
lakini kuna shows zangu ambazo nikipiga mpunga napiga pesa ya maana sana
(anacheka).” Mwasiti ameiambia Hisia.
“Kuna vijana wanapenda sana Zouk Rhumba huwezi amini. Na kuna wa umri
fulani sasa wale wa miaka 35 kwenda juu wanapenda sana Zouk Rhumba, kwa
hiyo wale huwa wana corporate shows, viongozi na nini.
“Kwa hiyo mara nyingi nafanya hizo sana kuliko zile za uwanjani
ambazo wengi wanategemea kuniona, za vijana zaidi. Kibiashara iko vizuri
as long as unatoa kazi ambayo wataielewa.” Ameongeza.
Mwasiti anatarajia kuachia nyimbo mbili hivi karibuni. ‘Leo’ aliomshirikisha Godzilla na ‘Kisigino’.
Post a Comment