Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba, ambaye pia ni mwanasiasa mkongwe nchini ,
Mzee Kingunge Ngomabale Mwiru amesema Katiba bora ni ile
itakayozingatia historia mafanikio ya miaka 50 iliyopita na Muungano
imara.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Mzee Kingunge wakati akichangia katika mjadala wa Bunge hilo juu ya uwasilishaji
wa taarifa za Kamati Namba Moja hadi Kamati Namba Kumi na Mbili za
Bunge hilo kuhusu uhakiki wa Rasimu ya Katiba iliyopendekezwa.
Aidha Mzee Kingunge amesema wameondosha mapendekezo ambayo yanataka kusambaratisha muungano ili uweze kuwa imara.
Mzee
Kingunge aliyataja mambo matatu ambayo yatazingatia Katiba bora kuwa
ni ni ile itakayoimarisha historia ya mafanikio ya miaka 50 iliyopita,
inayopunguza na kuondoa kero mbalimbali za msingi.
Aliongeza
kuwa tatu ni “Lazima Katiba Mpya iingize mambo ambayo yataimarisha
nafasi za wananchi mfano wakulima , wafugaji, wavuvi, wasanii na
wachimbaji wadogo… Tanzania haitakuwa kama ilivyokuwa huko nyuma baada
ya mkutano huu.
“ Kwa sababu makundi yote yote yamekutana hapa kuzungumzia maslahi yao na hatma yao,” alisema Mzee Kingunge.
Mzee Kingunge alisema mawazo yaliyotolewa na ni ushindi mkubwa, kazi iliyobaki ni kupitisha.
“Kazi hii si ndogo ni kubwa…kwani kuna zogo
, lakini tumevulia napenda iandikwe kwa wino wa dhahabu kama ilivyo hapa ndani,” alisisitiza.
Mwanasiasa
huyo alifafanua kuwa Katiba ni maridhiano, hivyo anajua wakubwa
wataendelea kuzungumza, hivyo katika hilo ni vizuri wakawa waangalifu.
“ Tuifanye kazi hii kwa unyenyekevu, wananchi wanangoja Katiba bora,” alisema.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalum la
Katiba,Mhe. Andrew Chenge alisema wakati akihitimisha mjadala huo, si
rahisi kuweka mambo yote kama yalivyotolewa na baadhi ya wajumbe wa
Bunge hilo, bali itachukua yale ya msingi mengine yatazingatiwa katika
Sheria za Nchi.
Aliwaasa
Watanzania kuisoma Rasimu ya Katiba Mpya iliyopendekezwa na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba na ile Rasimu ya Katiba Mpya iliyopendekezwa na
Bunge hilo.
Ninyi ndio mtakaoamua ukweli uko wapi? Tumeboresha hakuna kazi ya kuweka koma tumekuja kuandika Katiba ya Watanzania.
Mhe. Chenge alisema Kamati yake ni wajumbe ambao ni hazina kwa Tanzania.
Kwa
upande wake, mjumbe wa Bunge hilo, Mhe. Profesa Mark Mwandosya alisema
kazi iliyofanywa na Bunge hilo imefanywa kwa uadilifu, hivyo
wamezingatia Rasimu ya Katiba Mpya ya Tume na wameboresha kwa
kuzingatia maslahi ya wananchi.
Post a Comment