
Habari
zilizotufikia hivi punde zinasema Jeshi la polisi mkoani Geita
limekamata bunduki saba (pichani) na mabomu kadhaa ya machozi eneo la
Ushirombo wilaya ya Bukombe ikisadikiwa kuwa ni kati ya bunduki kumi
zilizoporwa na majambazi yaliyovamia kituo cha polisi Bukombe na kufanya
mauaji ya askari polisi wawili waliokuwa zamu jana. Bunduki hizo, nne
zikiwa SMG na tatu aina ya Shotgun pamoja na panga zimepatikana katika
tanuri la kuchomea matofali zikiwa zimefichwa pamoja na mabomu hayo.
Habari
zinapasha pia kwamba katika msako huo mkali unaoendelea, Jeshi hilo pia
limewatia mbaroni watu wawili wanaohisiwa kuwa ni majambazi
yaliyohusika na shabulio hilo, mmoja akiwa kakutwa akiwa na bomu juu
ya mti, majira ya jioni ya leo.
Jeshi
la polisi nchini tayari limetangaza dau la shilingi millioni 10 kwa
mtu yeyote atakaye fanikisha kuwakamata au kuwabaini waliohusika na
vitendo hivyo. Taarifa zaidi tutaendelea kuwaletea kwa kadri
zitavyopatikana
إرسال تعليق