Bw.
Julius Mziray mkaguzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)
akizungumza na waandishi wa habari katika hospitali ya Regency ya jijini
Dar es salaam. Baada ya kumkamata mtu mmoja anayetuhumiwa kutumia kadi
ya bima ya afya yenye namba 02-HCTP1801 ambayo inamilikiwa na Bw. Terry J. Maona kinyume na utaratibu , Mtu huyo alikamatwa jana katika hospitali hiyo wakati akitaka kufanya vipimo vya (CityScan),
ndipo mmoja wa wafanyakazi wa hospitali hiyo alipogundua na kupiga simu
makao makuu ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuwataarifu
kuhusiana na tukio hilo, ambapo maofisa walifika na kukamata nyaraka
hizo huku mgonjwa akitokomea kusikojulikana baada ya kugundulika, Bw. Julius Mziray amewaasa
wamiliki wa kadi za Bima ya Afya kutozitumia watu tofauti badala yake
zitumie kwa wahusika walioorodheshwa katika bima hiyo tu Jambo ambalo
kuwaigiza katika mikono ya sheria na kupata adhabu kali.
Bw. Julius Mziray mkaguzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF akiwasomea waandishi wa habari maelezo yaliomo katika nyaraka hizo
Baadhi ya wgonjwa mbalimbali wakisubiri huduma katika hospitali hiyo
Baadhi ya wgonjwa mbalimbali wakipata huduma katika hospitali hiyo
إرسال تعليق