Rais wa Zambia ashindwa kuhutubia baraza la UN.

Rais wa zambia Michael Satta amelazwa hospitali mjini New York. Bwana Sata alikuwa New York kuhudhuria mkutano wa mwaka wa viongozi wa dunia katika baraza kuu la umoja wa mataifa ambapo alitakiwa kutoa hotuba yake Alhamisi.
Hakuweza kutoa hotuba hiyo kwa wanachama  193 wa taasisi hiyo ya dunia. Ofisi ya habari katika idara ya polisi mjini New York imewaambia waandishi wa habari alipelekwa hospitali Alhamisi lakini haikutoa maelezo zaidi  kuhusu ni hospitali gani wala hali ya bwana Sata.
Ofisi hiyo imethibitisha ripoti  kwamba madaktari wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani walimtibu bwana Sata mapema siku hiyo katika hoteli.
Rais huyo mwenye umri wa miaka 77 hajaonekana  hadharani  kwa takriban miezi mitatu kabla ya kuhudhuria ufunguzi wa  bunge la Zambia wiki iliyopita.
Mwanzoni mwa hotuba yake mjini Lusaka, bwana sata aliwaambia wabunge kwa utani “ bado sijafa.” Wasiwasi kuhusu afya ya bwana Sata  uliongozeka nchini Zambia tangu aliposafiri kwenda Israel kwa matibabu mwezi juni na baadae kujiondoa  kwenye  macho ya umma.
- V.A

Post a Comment

أحدث أقدم