Wakati Majeshi ya anga ya Marekani yakiendelea na
mashabulizi nchini Iraq na Syria kulenga kundi linalojiita Islamic
States of Iraq and Syris (ISIS), idadi kubwa ya wanajeshi wa Marekani
wamepinga hatua inayotaka kuchukuliwa na rais Barack Obama kupeleka
vikosi vya ardhini katika nchi hizo.
Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa na Military Times, 70% ya
wanajeshi wa vikosi vya ardhini waliohojiwa wamepinga upelekwaji wa
vikosi hivyo Iraq na Syria huku 25% tu ikiunga mkono.
Matokeo hayo yanatokana na uamuzi wa awali wa kupeleka vikosi vya
ardhini vya Marekani nchini Iraq katika harakati za kuung’oa utawala wa
Saddam Hussein ambapo wanajeshi wengi wa Marekani walipoteza maisha.
Chanzo: UStoday
إرسال تعليق