Sigombei Urais 2015 - Nkamia

Juma Nkamia akiongea na waandishi wa habari leo jijini Arusha katika studio za redio 5 zenye makao yake makuu.
Juma Nkamia akiongea na waandishi wa habari leo jijini Arusha katika studio za redio 5 zenye makao yake makuu.

Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Juma Nkamia ambaye pia ni Mbunge wa Kondoa Kusini (CCM) amesema kuwa hana mpango wowote wa kugombea nafasi ya Urais 2015 kama viongozi wengine wanavyotangaza nia na  kudai kuwa kazi yake kubwa ni kuhakikisha wananchi katika jimbo lake wanapata maendeleo kupitia nafasi yake ya ubunge.

”Pamoja na umri nilionao (42) sina mpango wowote wa kugombea nafasi ya Urais 2015. Umri usiwe kigezo cha kugombea. Uwezo wa kiongozi ni muhimu sana.” alisema Nkamia.

Waziri Nkamia aliyasema hayo leo mara baada ya kufanya ziara fupi katika kampuni ya Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Redio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha.
Jamii Blog: SIGOMBEI URAIS 2015 ASEMA NKAMIA

Post a Comment

Previous Post Next Post