[audio] Keissy tena! Akera Wazanzibar kuwaita 'mzigo' katika Muungano



Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ali Mohamed Kessy (kushoto) akiwakwepa wabunge wa CUF, Kombo Khamis Kombo (kulia) na Ibrahim Mohammed Sanya (wa pili kushoto) walipokuwa wakimfokea nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana na Mbunge wa Mikumi, Abdulsalaam Amer akijalibu kuwazuia. Picha ya mwezi Mei mwaka huu (picha: Edwin Mjwahuzi/MWANANCHI)


Maoni ya Mheshimiwa Mbunge Ally Mohamed Keissy (CCM, Nkasi) akitoa maoni yake kuhusu 'mzigo' wa Muungano wa Tanzania kwenye Bunge Maalum la Katiba ambapo Wajumbe kadhaa hasa wa kutoka Zanzibar walipaza sauti kusema kuwa 'anatukera' kwa kauli za maudhi.

Keissy alikejeliwa kuwa mwenyewe ni 'Mpemba', 'Mmanga', 'Mwarabu', 'Mgonjwa wa
akili akapimwe', na kadhalika na kushauri kuwa kwa nini asirudi kwao Uarabuni akapimwe, huku akirukia akisema anayemsema naye ni 'Mkongomani'.
Hii si mara ya kwanza kwa Mhe. Keissy kukera Wazanzibari, tunaweza kubofya hapa kurejea kero ya mwezi Mei

Post a Comment

Previous Post Next Post