Watafiti
wamechanganyikiwa kuhusu ikiwa kampuni ya Apple inapaswa kutoa kauli
yake kuhusu ripoti kuwa simu yake mpya ya iPhone 6 inajipinda mtumiaji
anapoishi kuiweka ndani ya mfuko wa suruale yake.
Watu kadhaa
ambao ni watumiaji wa iPhone 6 wamekuwa wakituma picha zao kwenye
mtandao wa MacRumors ambazo zineonekana kuonyesha simu zao zikiwa na
tatizo hilo.
Mwandishi wa habari kwenye mtandao wa 'Geek.com' pia aliripoti kuwa simu yake ye iPhone 6 imejipinda.
Na
haijulikani nini hasa kinachoifanya simu hiyo kujipinda, baadhi
wakisema huenda ni gamba lake ambalo limetengezwa kwa madini ya
Aluminium ambalo linaifanya rahisi kwa simu hiyo kujipinda.
Taarifa
za iPhone 6 kujipinda hazijaripotiwa tu kwenye blogu za habari za
kiteknolojia bali pia kwenye vyombo vya habari kama Independent, the
Washington Post, India Today na the Sydney Morning Herald.
Russell Holly, anayefanyia kazi mtandao wa habari wa geek.com,ni mmoja wa wale walioripoti kuwa simu yake imejipinda.
Watumiaji wa mtandao wa kijamii wa Twitter, wametu moani yao kuhusu habari za simu hiyo kujipinda.
BBC ilijaribu kuwasiliana na Apple kuhusu ripoti hizo lakini haijasema chochote mpaka sasa.
Mmoja
wa wataalamu wa maswala ya kiteknolojia, anasema kuwa kampuni ya Apple
inapaswa kuchunguza malalamiko hayo na hata kutoa taarifa rasmi haraka
iwezekanavyo.
Jasdeep Badyal anasema kuwa Apple inapaswa kujibu
madai hayo na kisha ikiwa ni kweli, basi inapaswa kuchukua hatua ya
kuwapa simu mpya watu walioripoti kuwa simu zao zimejipinda.
Aliongeza
kuwa hata kama kulikuwa na simu kdhaa tu zenye tatizo hilo, kampuni
hiyo inapaswa kutoa taarifa na kueleza kilichofanyika.


إرسال تعليق