Ujauzito wa rapper Witness waharibika, alikuwa amebeba mapacha

Ujauzito wa rapper Witness umeharibika na kupoteza mapacha aliokuwa anatarajia kuwapata.
1959220_10203127404337184_581002193_n
Akiongea na East Africa Radio, Witness ambaye ni mke wa mwanamuziki Ochu, amesema bado hajajua chanzo cha tatizo hilo. “Naendelea tu vizuri and I am just trying to be stronger. Sasa hivi ndio nimepata kidogo strength hata ya kuwaambia watu,” rapper huyo amekiambia kipindi cha Power Jams, Jumatatu hii.
“It was Friday and they were twins lakini I just don’t want to talk about it sababu bado sababu haijafahamika, so I am still checking some vipimo,” aliongeza.
Hiyo ni mara ya pili Witness kupata tatizo hilo.

Post a Comment

Previous Post Next Post