Kaimu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu kataka Wizara hiyo Dkt.
Deogratius Mtasiwa, akizungumza kwenye mkutano wa watendaji waandamizi
wa serikali kutoka katika Ofisi ya WaziriMkuu – Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) pamoja na waandishi wa habari kuhusiana
na Programu ya Utafutaji Fedha Nchini kwa maendeleo ya wananchi (Global
Local Finance Initiative (LFI) ambayo ilianza katika awamu ya majaribio
2012 na kuonyesha mafanikio. Kulia ni Mshauri Mkuu wa Ufundi wa
programu hiyo nchini Tanzania , Peter Malika.
Na Mwandishi wetu
Mfuko
wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, (UNCDF) umefurahishwa na
programu zinazoendeshwa nchini kwa msaada wake na kusema upo tayari
kuendelea kufanyakazi na serikali na wananchi wa Tanzania.
Kauli
hiyo imetolewa katika ziara ya Katibu Mtendaji wa UNCDF, Judith Karl,
ambaye anaitembelea Tanzania kwenye mkutano wake na watendaji waandamizi
wa serikali kutoka katika Ofisi ya WaziriMkuu – Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) jana.
Karl
ambaye ameongozana na Mkurugenzi wa Local Development Finance kutoka
Makao Makuu ya UNCDF, New York, David Jackson alisema wamefurahishwa
namna Tanzania inavyotekeleza mpango huo wa kuwezesha watanzania
kuchangia miradi yao ya maendeleo kwa kutumia vyanzo vya ndani katika
halmashauri mbalimbali.Miongoni mwa halmashauri zilizofanya vyema ni
Same na Kibaha.
Akiwa
na Mshauri Mkuu wa Ufundi wa programu hiyo nchini Tanzania , Peter
Malika, Mtendaji huyo alisema wamefika kutia saini mkataba wa maelewano
kati ya Tanzania na shirika hilo la Umoja wa Mataifa kwa lengo la
kutekeleza miradi 25 na hasa baada ya awamu ya kwanza wa miradi mitano
kuonesha mafanikio makubwa.
Akizungumza
Karl pamoja na kuelezea kazi za UNCDF nchini Tanzania alitangaza
kuanzishwa kwa Programu ya Utafutaji Fedha Nchini kwa maendeleo ya
wananchi (Global Local Finance Initiative (LFI) kwa mwaka 2014-2017,
ikiwa ni jitihada mpya ya UNCDF iliyoanzishwa kufuatia maarifa
yaliyopatikana katika utekelezaji wa LFI ya kwanza (Tanzania) katika
awamu ya majaribio (2012-2015).

Katibu
Mtendaji mpya wa Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa
(UNCDF), Bi Judith Karl akizungumza na baadhi ya wajumbe wa TAMISEMI
pamoja na waandishi wa habari juu Programu ya utafutaji fedha nchini kwa
maendeleo ya wananchi (Global Local Finance Initiative (LFI), ambapo
alitangaza kuizindua rasmi program hiyo katika mkutano uliofanyika
kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(OWM-TAMISEMI). Kulia ni Naibu Katibu Mkuu – OWM-TAMISEMI, Dkt.
Deogratius Mtasiwa.
Hadi
sasa, programu ya majaribio ya LFI nchini Tanzania inasaidia miradi 25
ya miundombinu iliyoanzishwa na wawekezaji wa umma na binafsi na ambayo
iko katika hatua mbalimbali za uendelezaji. Lengo la programu hiyo ni
kuanzisha makampuni makubwa ya uwekezaji katika halmashauri ili
kupunguza mchango wa serikali kuu katika mambo ambayo yanaweza kufanywa
na wananchi na wao wakabaki katika sera na mipango mikubwa.
Miradi
imetawanyika katika sekta mbalimbali zikiwezo za usindikaji bidhaa za
kilimo, nishati, miundombinu ya utoaji huduma za jamii, mawasiliano, na
uzalishaji viwandani, katika mikoa 10 kote nchini.
Miradi
mitano iliyopiga hatua kubwa zaidi inatarajiwa kufikia kikomo cha
bajeti yake katika miezi sita hadi tisa ijayo ambapo dola milioni 26 za
mtaji wa ndani katika muundo wa mkopo na misaada ipatayo dola milioni 3
ilihamasishwa.
Msaada
wa LFI kwa miradi ambayo iko katika muundo wa utaalamu wa kiufundi,
kutoa amana, misaada ya kifedha , mikopo ambayo inahitajika sana kwa
miradi midogo na ya kati ya miundombinu ili ivutie uwekezaji.
Matokeo
ya jumla ya LFI ni kuongezeka kwa ufanisi wa rasilimali fedha kwa ajili
ya maendeleo ya kiuchumi ya hapa nchini kupitia uhamasishaji kwanza
kabisa wa mtaji binafsi kutoka nchini na masoko ya mitaji ilikuwezesha
na kuhamasisha maendeleo ya mahali yaliyojumuishi na endelevu.

Mshauri
Mkuu wa Ufundi wa programu hiyo nchini Tanzania , Peter Malika,
Mtendaji akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ambapo
alisema kuwa lengo lake ni kutoa ushauri wa kitaalamu, fedha na namna ya
kuchagua miradi yenye tija katika jamii ili wananchi waweze kujiletea
maendeleo yao wenyewe na taifa kwa ujumla. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha
mawasiliano Serikalini-TAMISEMI, Rebecca Kwandu na kushoto ni Kaimu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu kataka Wizara hiyo Dkt.
Deogratius Mtasiwa.
Katika
mauzungumzo hayo ambapo Naibu Katibu Mkuu – OWM-TAMISEMI, Dk Deogratius
Mtasiwa alikuwepo, UNCDF imesema inatambua ushirikiano mzuri kabisa
uliotolewa na serikali kupitia OWM-TAMISEMI, hasa wajibu wake kama
mshirika katika utekelezaji wa programuya LFI na kusaidia kubaini na
kuendeleza miradi ya miundombinu inayofaa kwa biashara inayofadhiliwa na
mamlaka za serikali za mitaa.
Katika ziara yake Katibu Mtendaji huyo anatarajia kuona namna ya kupanua msaada wa UNDCF kwa Tanzania.
Misaada
hiyo ni pamoja na uanzishwaji wa huduma bunifu inayosaidia kuongeza
upatikanaji wa huduma za fedha na kujaribu njia za kufungua milango ya
mtaji wa mahali ili kuwekeza katika miradi ya maendeleo.
Shabaha
ya UNDCF ya kutoa mtaji wa uwekezaji na utaalamu wa kiufundi kwa sekta
ya umma na ya binafsi umelenga kuwezesha mikopo na uazimaji fedha wa
ngazi ya juu na utaalamu wa kiufundi katika kuandaa maandiko endelevu na
yenye manufaa ya kujenga uwezo na miradi ya miundombinu.
Aidha
UNCDF inaelekeza jitihada zake katika kuimarisha menejimenti ya masuala
ya fedha za umma na mapato ya mahali, kuimarisha ubora wa uwekezaji wa
umma na binafsi katika ngazi ya mahali.

Mkurugenzi
wa Local Development Finance kutoka Makao Makuu ya UNCDF, New York,
David Jackson akifafanua jambo kwa waandishi wa habari ambapo alisema
wamefurahishwa namna Tanzania inavyotekeleza mpango huo wa kuwezesha
watanzania kuchangia miradi yao ya maendeleo kwa kutumia vyanzo vya
ndani katika halmashauri mbalimbali. Kulia ni Katibu Mtendaji mpya wa
Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNCDF), Bi Judith Karl.
Kazi
ya UNCDF katika masuala ya fedha jumuishi inalenga kuendeleza mifumo ya
fedha iliyo jumuishi na kuahakikisha kuwa bidhaa mbalimbali za fedha
zinapatikana katika matabaka yote ya jamii, kwa gharama nafuu, na kwa
namna iliyo endelevu.
Lengo la asili la UNCDF – kuhamasisha maendeleo ya kiuchumi katika nchi zinazoendelea – linaendelea kuwa na maana hata leo.
UNCDF
wanaangalia ukuaji wa kiuchumi kama kitu muhimu katika kuongeza ubora
wa maisha, kupunguza umaskini na kuendana na idadi ya watu inayozidi
kukua.

Baadhi ya maafisa kutoka Umoja wa Mataifa wakiwa kwenye mkutano huo.

Katibu
Mtendaji mpya wa Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa
(UNCDF), Bi Judith Karl akipogezana na Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambaye pia ni
Naibu Katibu Mkuu kataka Wizara hiyo Dkt. Deogratius Mtasiwa baada ya
kuzinduliwa rasmi kwa program hiyo nchini. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha
mawasiliano Serikalini-TAMISEMI, Rebecca Kwandu na kushoto ni Mkurugenzi
wa Local Development Finance kutoka Makao Makuu ya UNCDF, New York,
David Jackson.

Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo.

Mtaalam
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce
Temu (kushoto) akibadilishana mawazo na Imanuel Muro kutoka UNCDF pamoja
na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Serikalini-TAMISEMI, Rebecca Kwandu
(katikati) mara baaada ya kumalizika mkutano huo.

إرسال تعليق