
Mkuu
 wa jeshi nchini Marekani Jenerali Martin Dempsey amesema kuwa 
mashambulizi ya angani dhidi ya kundi la Islamic State yameliharibu 
kundi hilo,lakini akaonya kuwa kampeni hiyo ya angani pekee haiwezi 
kuliangamiza kundi hilo.
Amewaambia waandishi habari kwamba kampeni ya nchi kavu dhidi ya kundi hilo ni muhimu nchini Iraq na Syria.
Jenerali
 Dempsey amesema kuwa kati ya wapiganaji elfu kumi na mbili na elfu kumi
 na tano kutoka kwa makundi ya upinzani nchini Syria watahitajika katika
 vita vya nchi kavu nchini Syria.
Idadi hiyo ni mara mbili na hata
 tatu kwa ukubwa ukilinganisha na idadi inayotarajiwa kupewa mafunzo ya 
kijeshi mbali na silaha na wanajeshi wa Marekani.
إرسال تعليق