Viongozi
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Katavi na
wafuasi wake 16 wa wanashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za
kufanya maandamano bila kibali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi
Dhahari Kidavashari alisema kuwa viongozi hao walikamatwa Septemba
25,majira ya saa 11.30 asubuhi mtaa wa majengo mkabala na nyumba ya
kulala wageni ya Dubai Kata ya Kashaulili Wilayani Mpanda.
Viongozi hao na waafuasi wao
walikamatwa baada ya kufanya Maandamano bila kibali kwa ajili ya
kuunga mkono maagizo yaliyotolewa na Viongozi wao wa Kitaifa ya kufanya
maandamano nchi nzima kwa lengo la kuishinikiza Serikali isitishe
Kikao Maalumu cha Bunge la Katiba na kusitishwa kwa Rasimu ya Katiba
Mpya.
Wanaoshikiliwa na Polisi ni
Almasi Ibrahim Ntije Katibu wa Chadema wa Mkoa wa Katavi, Abrahma
Mapunda (16),Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Mpanda,Hamisa Kolongo
(60) Katibu wa Chadema Mpanda.
Wengine waliokamatwa ni Lameck
Constantino (37) Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Mpanda na Mkazi wa
Itenka, Mlokozi Bagasheki (30) Mwenyekiti wa Vijana Cretus Aloyce
(320Katibu wa Jimbo la Mpanda na Shabani Ibrahimu (26)Katibu wa Vijana
Chadema na mkazi wa Kotazi.
Mbali ya viongozi hao pia wafuasi
wengine waliokamatwa ni Kenedy Zakayo (20) mwanachama mkazi wa kijiji
cha Ilebula,Mariam Omary (43)Katibu muenezi wa Chadema, mkazi wa
majengo,Fransisco Misigalo (29) mwenyekiti wa vijana Mkoa Mkazi wa
Kashaulili,Selemani Hamisi (25) mkulima wa misunkumilo.
Wengine waliokatwa ni Anselemu
Kanyengele (45) mkazi wa Majengo, Kasena Maulid Mjumbe wa Chadema
Wilaya,Mwailwa James (35) mwanachama na mkazi wa kotazi, Emil Kalomo(30)
mkulima,na Seif Ibrahimu(34) mwanachama na mkazi wa Majengo.
Taarifa zilizopatikana kutoka kwa
viongozi wa chama hicho walieleza kuwa awali Chama hicho kiliandika
barua hapo Septemba 22 kwa jeshi la polisi wakiomba kufanya maandamano
tarehe 25 pamoja na Mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Mpanda Hoteli
Hata hivyo barua hiyo ilijibiwa
na jeshi la Polisi Wilaya ya Mpanda hapo Septemba 24 ikikitaka
Chama kisifanye Maandamano wala Mkutano wa hadhara.
Kwa mujibu wa Maelezo ya Katibu
wa Chadema wa Wilaya ya Mpanda Idd Faraja alieleza kuwa Chama
kiliamua kufanya maandamano hayo baada ya kufanya maandalizi ya
maandamano hayo na jeshi la polisi kuchelewa kuwapatia barua ya
kuwazuia kufanya maandamano na mkutano.
Akaeleza kuwa kitendo cha Jeshi
laPolisi kuchelewa kujibu barua yao ya kuomba kibali walivyoona
imekuwa kimya walijijua kuwa wamekubaliwa.wakaamua kufanya maamuzi ya
kuandamana bila kibali.
Katika Hatua nyingine Ofisi za
Chadema ambazo zipo katika Mtaa wa Majengo A’ jana kutwa nzima
zilishinda zimezungukwa na Askari wa Jeshi la Polisi waliokuwa na silaha
chini, PIA Kituo Kikuu cha Polisi Wilaya ya Mpanda kiliimalishwa kwa
Ulinzi baada ya kuwepo ulinzi kuhofiwa kuvamiwa na wafuasi wa Chadema
walioonekana kuwa na hasira.
Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Katavi Dhahari Kdavashari amewatahadharisha wananchi na wakazi wa Mkoa
huo wa Katavi kutojihusisha na maandamano ya namna yeyote ya Kisiasa
hadi hapo yatakaporuhusiwa.
Pia amewaasa kutoshawishiwa na
chama chochote kushiriki maandamano au migomo kwani watakuwa wamekiuka
sheria na taratibu za nchi.

إرسال تعليق