Utafiti unaonyesha kuwa wanawake wanaonenepa maishani bila ya kuwa waangalifu wanajiweka katika hatari ya kupata Saratani.
Watafiti
kutoka chuo Kikuu cha London wanasema kwamba wanawake walio kati ya
umri wa miaka 24-28 ambao huendelea kunenepa kila baada ya miaka 10,
wako katika hatari zaidi ya kupata Saratani ya Matiti baada ya kupitisha
umri wa kuzaa.
Sasa je ni nini ishara ya mwanamke kunenepa?
Watafiti wanasema vipimo vya sketi yake vinaweza kukusaidia kujua ikiwa
uko katika hatari ya kpatwa Saratni ya Matiti au la.
Kila
unapogundua kuwa sketi yako inaendelea kuwa ndogo kiunoni, basi
inakubidi ujue kuwa mwili wako unaongekeza kwa unene. Na pia ni rahisi
kwa wanawake kukumbuka kipimo cha sketi kuliko kitu kingine chochote.
Kwa
hilo watafaiti wanasema mwanampe anapaswa kutahadhari kila sketi yake
inapoendelea kuwa ndogo kwake maana kwamba amenenepa zaidi. Ikiwa ukubwa
wake unazidi kwa kipimo cha sketi mbili katika kipindi kimoja basi
mwanamke anakuwa katika hatari ya kupatwa na Saratani hata zaidi.
'Mfumo wa maisha'
Akizungumzia utafiti huo, Simon
Vincet kutoka shirika la kupambana na saratani ya Matiti la
Breakthrough Breast Cancer, alisema kuwa saratani ya Matiti miongoni mwa
wanwake inaweza kupunguka ikiwa watu watabadilisha mfumo wa maisha kwa
kujiuzia kunenepa kupita kiasi na kufanya mazoezi sana.
Utafiti huu unaangazia njia rahisi sana kwa wanawake kuwa waangalifu kuhusu unene wa miili yao.
Kuangalia
kipimo cha sketi kati ya wanawake walio kati ya miaka 24 na 28 wenye
miaki katikati ya 20 na zaidi wanaweza kuwa na njia rahisi ya kufuatilia
uzito wa miili ya Unene wa kupita kiasi unajulikana kwa sababu ni
hatari kubwa inayochangia katika ugonjwa wa saratani , hususan mafuta ya
yaliyoko tumboni.
Prof Usha Menon wa shirika lakupambana na
satratani ya matiti, ndiye aliyeongoza utafiti huo na kuambia BBC kuwa
"Kama kipimo cha sketi kinaweza kuthibitishwa na wengine kama kigezo cha
wanawake watu wazima kuapa Saratani, basi hii itakuw anjia nzuri na
rahisi ya mtu kuwa mwangalifu ili asinenepe kupita kiasi.
'Changamoto'
Watafiti hao walisema utafiti
wao ulikuwa na changamoto kadhaa kwamba uliangazia zaidi wanawake
kukumbuka vipimo vya sketi zao tangu tangu wawe na umri wa miaka 20
Lakini
ikiwa matokeo ya utafiti huo yatathibitishwa, itakuwa njia rahisi kwa
wanawake kuelewa hatari zinazowakabili hasa wanapoendelea kunenepa.
Tom
Stansfeld kutoka shirika la utafiti wa Saratani nchini
Uingereza,anasema utafiti huo unaweza kuaminika lakini unazingatia zaidi
wanawake kukumbuka vipimo vya sketi walizovalia miaka ya zamani.
Utafiti
unasema kuwa baadhi ya mambo muhimu ambayo mwanamke anaweza kufanya
kupunguza tisho la kuugua Saratani ya Matiti , hasa baada ya kupitisha
miaka yake ya kuzaa ni pamoja na kufanya mazoezi , kula vizuri na
kupunguza ulevi.
Kupunguza unene ni njia moja wapo ya kupunguza
tisho la kupata Saratani baada ya kupitisha miaka ya kuzaa na kuangalia
vipimo vya sketi za wanawake kuwahamasisha wanawake.
إرسال تعليق