
Idadi ya watoto wa familia moja
waliokufa kwa ajali ya moto katika nyumba ya wazazi wao waliyokuwa
wakiishi, mkoani Geita, imeongezeka kutoka watatu hadi wanne, baada ya
mmoja wao aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando, mkoani
Mwanza, kufariki dunia.
Mtoto huyo, Scolastika (15),
ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya
Mwatulole, alizikwa Septemba 14,2014.
Alisema alimwambia mkewe,
Angelina Gasper, wapige magoti na kuomba nusura ya Mungu baada ya moto
huo kuzuka katika nyumba wanayoishi.
Nyumba hiyo iliteketezwa usiku wa Septemba 7, mwaka huu, baada ya watu wasiofahamika kuimwagia mafuta ya petroli.

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Manzie Mangochie.
Watoto
wengine waliotetekea katika ajali ya moto huo, ni Reginald Robert (9),
ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne na Sofia (6) wa Shule ya Msingi
Ukombozi na Remijius (4) wa Chekechea, walifariki papo hapo.
Mkewe, Angelina akizungumza kwa
shida kutokana na kuondokewa na watoto wake wanne, alisema huo si msiba
zaidi ya msiba, kutokana na kubakiwa na watoto wawili kati ya sita,
ambao wanne wakifariki katika tukio hilo.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya
Wilaya, Dk. Adam Sijaona, alisema kuwapo kwa tukio hilo kumemfanya
akutane na mkasa, ambao hajawahi kukutana nao.
Afisa Mtendaji kata ya
Kalangalala, Hamad Hussein, alisema waliotenda tukio hilo walimimina
mafuta ya petroli milangoni na madirishani na kuilipua nyumba hiyo
iliyoezekwa kwa bati inawezekana kwa chuki binafsi ama migogoro ya
ardhi.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa
huo, Hassan Mcharo na Afisa Mtendaji wa Mtaa huo, Simfukwe Ally, kwa
pamoja wamelaani tukio hilo wakati wakizungumza na gazeti hili juzi.
Mkuu wa Wilaya ya Geita, Manzie
Mangochie, akizungumza kwa masitikiko kuhusu tukio hilo, alisema
amesikitishwa na kitendo hicho na kuagiza kuhakikisha kuanzia ngazi ya
mtaa hadi wilaya wanashirikiana kuhakikisha waliohusika na unyama huo
wanakamatwa.
إرسال تعليق