Kijana mmoja ameshambuliwa na kundi la wazee alipokaidi kumwachia kiti mmoja wao ndani ya basi nchini China.
Katika
mabasi yanayoelekea eneo la Wuhan, viti vyake vya njano vina maana
maalum, kutokana na kwamba viti hivyo vimetengewa wazee, anawake
wajawazito ama wagonjwa.
Hata hivyo heshima hiyo imekuwa ikivunjwa ama kukiukwa hasa na vijana.
Lakini
kijana mmoja aliyeamua kukaa katika moja ya viti hivyo visivyomuhusu,
alionja joto la jiwe baada ya kupewa kipigo na wazee wenye haki ya kukaa
katika siti hizo.
Mzee mmoja aliyekaa na kijana
huyo alimtaka asimame na kuachia nafasi hiyo ili ampishe mzee aliyekuwa
amesimama, lakini kijana huyo alikaidi na ndipo mtafaruku ukaanza kwa
kushambuliwa na wazee waliokuwamo katika basi hilo.

إرسال تعليق