Shirika
 la afya duniani limesema kuwa zaidi ya watu elfu tatu sasa wamedaiwa 
kufariki kutokana na kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola katika eneo la Afrika 
Magharibi kati ya visa elfu sita vya ugonjwa huo vilivyoripotiwa.
Liberia
 imeathiriwa vibaya na ugonjwa huo huku WHO ikisema kuwa kumekuwa na 
vifo 150 vilivyotokea katika kipindi cha siku mbili pekee.
Idadi hiyo inaweza kupuuzwa kwa kuwa watu wengi wanaogopa kwenda hospitalini.
Hazina ya Fedha duniani IMF imeahidi dola millioni 130 kama msaada wa dharura kwa mataifa ya Liberia,Guinea na Sierra Leone.

إرسال تعليق