Hundi ambazo siyo sahihi kwa malipo ya
waliopoteza nyumba wa watu na mali huu siyo Ubinadamu madaraka yana mwisho.
Wanasikitika kwa kutotendewa haki ya
kibinaadamu.
Wananchi wa Mbagala Kuu Waathilika na
Mabomu wanaamini wametolewa Kafara kwa viongozi waliosimamia malipo kwa
kunufaika kupitia matatizo yao.
Mh. Rais wananchi wanasema toka
ulipokwenda mbagala Kuu februari 2010 hakuna kilichofanyika zaidi kulipwa kiasi
cha Tsh 1,400 na 1950 fidia ya nyumba je hii ndiyo HAKI? Rais.
Wakiwa na mabango yenye ujumbe wa
kulalamikia malipo ya dhuluma.
Wananchi wa Mbagala Kuu ambao waliathilika na
mlipuko wa mabomu katika kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ), Aprili 2009
wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kumtaka Rais Jakaya Kikwete asikilize kilio
chao baada ya kufanyiwa unyama na viongozi waliosimamia zoezi la malipo yao.
---
Na Asha Mwakyonde
ZAIDI ya waathirika 1000 wa milipuko ya mabomu
ya Mbagala Kuu iliyotokea jijini Dar es Salaam mwaka 2009, wanatarajia kuitisha
mkutano wa hadhara wa kuwaondoa madarakani viongozi wao wa serikali ya mtaa kwa
madai ya kushindwa kusimamia madai ya kupunjwa fidia ya majengo.
Wamesema licha ya miongoni mwao kulipwa fidia ya
shilingi 1,400 kwa nyumba bado viongozi wao wa mtaa wameendelea kuwa
kimya katika kufuatilia fidia halisi tangu janga hilo la mabomu liwakute miaka
minne iliyopita.
Wakazi hao wa Mbagala Kuu, walitoa kauli hiyo
jana walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari na kusema wamefikia uamuzi
huo baada ya kukosa imani na viongozi wao.
Akizungumza kwa niaba ya waathirika wa mabomu
hayo katibu wa Kamati ya Waathirika, Thomas Mbasha, alisema madai yao ni pamoja
na kulipwa fidia ndogo na kwamba hata baada ya kuandika barua ya malalamiko
kwa serikali wakitaka kuongezwa fidia lakini hawajapata majibu yenje
tija.
“Tumeandika barua kadhaa kwa serikali ikiwa ni
pamoja na Rais tukiomba fidia zetu lakini hakuna kilichofanyika,tunahitaji Rais
aingilie kati suala hili na kutusaidia ili tulipwe stahili zetu kabla
hajaondoka madarakani,” alisema Mbasha.
Alisema fidia walizolipwa awali hazilingani na
thamani ya mali na vitu walivyopoteza wakati wa mabomu hayo huku akiainisha
fidia ya kiwango cha juu walicholipwa ni shilingi 4900 .
Awali Mwenyekiti wa Kamati ya waathirika
wa mabomu ya Mbagala kuu, Stephen Gimonge, alisema Rais Jakaya Kikwete,
alitembelea eneo hilo na kuahidi kuwa serikali itawalipa fidia inayostahili
lakini ahadi hiyo haijazaa matunda.
Alisema wakati wa ziara yake kwa waathirika wa
milipuko ya Mbagala Rais Kiwete alimuelekeza Waziri Mkuu kuhakikisha fidia
inatolewa kulingana na mali zilizopotea.
Hata hivyo waathirika hao walimuomba
Kikwete kuingilia kati ili awasaidie waweze kupata fidia inayostahili kutokana
na mali na vitu vyao vilivyoharibiwa wakati wa tukio hilo lililotokea Aprili
2009.
Post a Comment