Wasanii
chipukizi kutoka morogoro watembelewa
katika vijiwe vyao na kujiunga na
mashindano ya Airtel Trace
Kampuni ya simu za mkoni ya Airtel imeendelea
kuwafikishia wateja wake na wapenzi wa muziki katika mikoa mbalimbali na
kuwaunganisha katika mashindano ya kutafuta mwamamuziki chipukizi ya Airtel
Trace yaliyozinduliwa rasmi nchini mwanoni mwa mwezi octoba. Airtel imetembelea
Mkoa wa Morogoro na kuzindua rasmi huduma ya Airtel Trace music star katika
vijiwe mbalimbali mkoani hapo
Akizungumza na wasanii chipukizi wa muziki wa
kizazi kipya katika vijiwe mbalimbali mjini Morogoro, Meneja uhusiano wa Airtel
Jackson Mmbando amesema huduma hiyo inamuwezesha mtu yeyote mwenye kipaji cha
kuimba kujiunga na kushiriki kwa kupitia simu ya mkononi kwa kupiga namba
0901002233
kisha kurekodi wimbo wake na kuutuma
Mashindano haya yanatoa mwanya wa watanzania
wenye ndoto za kuwa wanamuziki nyota kupata fulsa ya kuzifikia ndoto zao.
Sambamba na hilo tutakuwa na washindi watakaojishindia zawadi mbalimbali hapa
nchini kama vile pesa taslimu na nafasi ya kushinda na kushiriki mashindano ya
Afrika yatakayofanyika nchini south Afrika na kushirikisha washindi wengine
toka nchi 13 barani afrika ambabo Mshindi wa Afrika atapata nafasi ya nafasi
kwenda kurekodi wimbo wake nchini Marekeni na kupata mafunzo ya muziki kutoka
kwa msanii nguli wa muziki Akon huko nchini Marekani
Nao baadhi ya wasanii waliokutwa kwenye vijiwe
vyao waliweza kushiriki shindano hilo kwa kurekodi nyimbo zao kupitia Airtel
Trace muziki star huku wakiishukuru Airtel kwa kuwaletea huduma ambayo
itawakomboa wasanii chipukizi wasio na uwezo
Ambapo Hamis Ramadhan aka brash waya 2
alikuwa na haya ya kusema” tunashukuru Airtel kwa kutuletea mshindano haya
kitaani kwani tunavipaji lakini tunashindwa kupiga hatua kwakuwa uchumi ni
mdogo tunaamini kwa kuppitia Airtel Trace tutatoka , kukubwa ni kusaidia na
kupigiana kura ili tufanikiwe, tunaamini Airtel Trace Tanzania Atatokea
Morogoro na hivyo natoa wito kwa wanamorogoro wajiunge kwa wingi na kutumia
nafasi hii ili kubuka kuwa masuper star
Kwa upande wake Ramadhani Nguyao alisema “
nimefurahia mpango mkubwa na wakwanza Tanzania utakaowawezesha wasanii
chipukizi kupata fulsa ya kuimba na kurecord wasanii wakubwa kama Akon. Mimi
nimevutia na ntajiunga na mashindano haya na waomba watanzania wengi na
wasanii wenzangu wa Morogoro na nje ya Morogoro kujiunga na kushiriki katika
mashindano haya ya Airtel Trace Music Stars.
Mashindano ya Airtel Trace Music Stars
yalizinduliwa rasmi nchini Mwanzoni na October na yatadumu kwa muda wa mienzi
sita ambapo fainali ya mashindano haya inategemea kufanya Mwaka kesho Machi
2015 nchini South Afrika.
Post a Comment