Muuaji wa Meyiwa ni Kitendawili

Senzo Meyiwa enzi za uhai wake
Polisi nchini Africa Kusini wameanzisha msako mkali dhidi ya mtu aliyempiga risasi na kumuua kipa na kapteni wa timu ya taifa hilo Senzo Meyiwa.
Ili kufanikisha na kuufanya uchunguzi wao uwe rahisi na wa haraka,polisi hao wametoa zawadi nono ya randi 250,000 sawa na dola za kimarekani 14,000; hadi $23,000 kwa yeyote atakayefanikisha taarifa za kukamatwa kwa mtu huyo,ambaye anaongeza namba ya matukio ya uhalifu yaliyokithiri nchini humo.
Meyiwa, amekufa akiwa na umri wa miaka 27, inaarifiwa kuwa alipigwa risasi na kuuawa na mtu aliyeingia nyumbani kwa mpenzi wake na kutekeleza mauaji hayo.
Rais wa taifa hilo Jacob Zuma ametuma salamu za rambi rambi na kutoa ujumbe kwamba maneno hayatoshi kuonesha mshtuko wa taifa letu kwa kuuawa kwa Meyiwa.
Polisi wametoa taarifa kuwa si mtu mmoja bali walikua wanaume wawili waloingia nyumbani na mmoja alibaki nje ya nyumba hiyo huko kwenye kitongoji cha Vosloorus,jijini kusini mwa Johannesburg,na walipoingia wakadai Meyiwa .
Rais Jacob Zuma amesema kwamba taifa lake linaomboleza kifo cha mchezaji nguli na mchanga na kiongozi wa timu ya taifa ambaye maisha yake yamepokwa angali mdogo na katika kilele cha mafanikio yake , na maneno pekee hayatoshi kuelezea hasara waliyopata.
Vituo vya redio na runinga vina pokea ujumbe wa pole kwa kifo cha Meyiwa .
Tukio hilo la kupigwa risasi kwa Meyiwa kunaonesha taswira ya matumizi mabaya ya silaha nchini Africa Kusini, ikiwa ni siku chache tu kesi ya mwanariadha Osca Pistorious iliporindima nchini humo na kutolewa maamuzi ambayo hayajawaridhisha walio wengi nchini humo.
Taifa hilo linajiuliza maswali lenyewe juu ya kuongezeka kwa matukio ya uhalifu nchini humo,na wanaouawa ni watu wenye vipaji vya kipekee kama miaka saba iliyopita aliuawa nguli wa muziki wa reggae Lucky Dube .
Jambo kubwa na la msingi kwa sasa dunia imewageukia wanamgambo wa kiislamu,wakati kuna uhalifu duniani kote.
Meyiwa alizaliwa mnamo tarehe 24 September ,mwaka 1987
Alikuwa ni kipa wa timu kutoka Johannesburg ya Orlando Pirates
Alijiunga na timu ya taifa hilo mwaka 2013
Mwaka uliofuata alichaguliwa kuwa kapteni wa timu ya taifa.
Na kuilete nchi yake vikombe saba vya ushindi alikuwa na mpenzi ambaye ni muigizaji Kelly Khumalo ambaye alipata naye motto mmoja naye.
Meyiwa anatajwa kuwa kipa bora barani Africa .

Post a Comment

Previous Post Next Post