ALI KIBA AKANUSHA KUANDAA WATU WAMZOMEE DIAMOND KWENYE FIESTA


Msanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba akifanya yake katika Tamasha la Serengeti Fiesta Leaders Club lilifanyika hivi karibuni.
Msanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba amekanusha uvumi unaodai kuwa huenda aliaandaa watu maalum wa kumzomea msanii Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' kwenye shoo ya Fiesta iliyofanyika October 18 katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.

Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz'.
Msanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba ameuambia mtandao wa  Bongo5 jana kuwa hahusiki na vurugu za mashabiki kumzomea msanii mwenzake, Nasibu Abddul 'Diamond' kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta lililofanyika wikiendi iliyopita katika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar.
“Hamna ukweli wowote, naanzaje?,” amehoji. “Siwezi kufanya kitu kama hicho. Kikubwa ni kuwashukuru wana Dar es Salaam walivyonipokea, nimefurahi sana. Hii imenitia moyo na kunifanya niongeze bidii kuwaandalia vitu vizuri zaidi.”
Katika hatua nyingine, msanii huyo amesema mashabiki wa muziki wake wasishangae kuona video ya wimbo wa ‘Mwana’ wiki hii ama wiki ijayo. “Video ni muda wowote yaani, usishangae ukasikia video imetoka. Muda wowote video inatoka surprise, kwa hiyo waendelee kusubiri muda wowote.”

Post a Comment

أحدث أقدم