HABARI njema kwa mashabiki wa Manchester United ni kwamba Angel di Maria yuko fiti kuivaa Chelsea Jumapili hii.
Mkali
huyo aliyesajiliwa kwa pauni milioni 60 kutoka Real Madrid, aliumia
mguu katika mechi ya 2-2 dhidi West Bromwich Albion Jumatatu na
ilihofiwa kuwa atakasa mchezo huo mkubwa wa kwanza kwake msimu huu.
Alifungwa
barafu mguuni baada ya kutolewa dakika ya 76 lakini ameweza kufanya
mazoezi siku mbili zilizopita na yuko fiti kuivaa Chelsea.
Naye
kiungo Michael Carrick aliyekuwa nje ya dimba kwa miezi mitano,
anatarajiwa kucheza katika mchezo huo hii ikiwa ni baada ya kujumuishwa
katika orodha ya wachezaji wa akiba Jumatatu iliyopita katika mchezo
dhidi ya West Bromwich Albion.
Post a Comment