MSHAMBULIAJI
mwenye kasi ya ajabu Theo Walcott amerejea kwenye kikosi cha Arsenal na
anajiandaa kwa safari ya kwenda kuikabili Sunderland baada ya goti
kumweka nje ya dimba kwa miezi tisa.
Walcott,
25, amecheza kwa dakika 45 katika mechi ya vijana wa chini ya miaka 21
Ijumaa iliyopita na anaweza akajumuishwa kwenye safu kali ya
ushambuliaji sambamba na Danny Welbeck na Alexis Sanchez ambayo itakuwa
safu ya ushambuliaji yenye kasi zaidi katika Premier League.
Post a Comment