Mtu
asiyefahamika akiwa ndani ya gari lake mara baada ya kupigwa risasi
tumboni. Kushoto kwake ni mwanamke aliyekuwa naye garini.
....wapita njiawakijaribu kutoa msaada kwa mtu huyo.
Muonekano wa nyumba wa gari hilo.
...hawa jamaa nao waligongana, mwendesha pikipiki na mwenye gari katika eneo la tukio na kuanza 'kuzikunja'.
Mtu mmoja ambaye hakuweza kujulikana jina lake mara moja amepigwa
risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi na kuporwa mkoba uliyokuwa
garini ambao haukujulikana ulikuwa na nini ndani yake. Tukio hilo
limetokea leo majira ya mchana maeneo ya Magomeni Mikumi jirani na kwa
Sheikh Yahaya jijini Dar es Salaam. Mtu huyo alipigwa risasi tumboni
akiwa kwenye gari yake Toyota Mark II (GX 100) yenye namba za usajili
T487 AZW. Kwenye gari hiyo, alikuwemo mwanamke mmoja akiwa amekaa kwenye
kiti cha mbele cha abiria ambaye hakujeruhiwa.
PICHA: HANS MLOLI/GPL
إرسال تعليق