Jeshi la polisi nchini Tanzania limewafukuza kazi maafisa wake watatu
kwa kosa la kupiga picha ya aibu na kuiweka kwenye mitandao ya kijamii.
Kamanda wa polisi mkoa wa
Kagera, kaskazini magharibi mwa Tanzania Henry Mwaibambe ameiambia BBC
kuwa askari hao wamekiuka maadili ya kazi yao pamoja na kulidhalilisha
jeshi hilo kwakuwa walipiga picha hiyo wakiwa wamevaa sare za jeshi
kinyume na sheria.
Askari hao walikuwa kazini wakati wakipiga
picha hiyo ambayo ilipigwa na askari mwenzao ambaye pia amefukuzwa kazi,
kama ambavyo kamanda huyo alivyosema kwenye mahojiano na mwandishi wa
BBC Baruan Muhuza.
Post a Comment