KINANA ATUA MUFINDI AWATAKA VIONGOZI KUTOJIPENDELEA KUPATA TENDA


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara, Uwanja wa Mashujaa mjini Mafinga, wakati wa ziara yake katika Jimbo la Mufindi Kaskazini, Iringa, ikiwa ni mwendelezo wa kuiamarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Kinana aliwataka viongozi kutokuwa na tamaa ya kuwa kiongozi na wakati huo huo kutaka kuwa matajiri pia aliwataka kuacha kujipendelea kujipa tenda badala ya kuwapatia kwanza wananchi.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamoud Mgimwa akihutubia na kuelezea miradi mbalimbali iliyotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010 katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini Mafinga leo.
 Kinana akiangalia mashine za kupasua mbao katika kiwanda cha mtu binafsi cha Emanuel, mjini Mafinga, Mufindi.
 Kinana akiwa na mkurugenzi wa kiwanda binafsi cha mbao cha Emanuel, Charles Akyoo alipotembelea kiwanda hicho leo.
 Kinana akitembelea kiwanda hicho wakati wa ziara yake katika Jimbo la Mufindi Kaskazini.
 Kinana akiangalia mti uliostawi vizuri uliopangwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, Baba wa Taifa Julius Nyerere 1989 katika Ofisi za Sao Hill, Mafinga
 Kinana akipanda mti wa kumbukumbu katika viwanja vya ofisi ya Sao Hill, Mafinga, wilayani Mufindi leo
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akipanda mti wa kumbukumbu katika viwanja vya Ofisi za Sao Hill, Mafinga
 Kinana akiwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya Mufindi,  Dk. Boaz Mnenegwa alipotembelea wodi ya wazazi katika hospitali hiyo wakati wa ziara yake, Jimbo la Mufindi Kaskazini.
 Wajumbe wa mkutano wa halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Mufindi, wakipiga makofi kumlaki Katibu Mkuu wa CCM, Kinana katika mkutano huo.
 Kinana akihutubia katika mkutao huo wa halmashauri
 Katibu wa Bakwata Wilaya ya Mufundi, Idrisa Witala akuuliza swali wakati wa mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na viongozi wa dini.
 Nape akishuka jukwaani baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mashujaa, Mafinga leo
 Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu akihutubia katika mkutano huo ambapo aliwaomba wazee, vijna, walemavu, wananwake na wasanii kuipigia kura ya ndiyo rasimu ya katiba iliyopitishwa hivi karibuni  katika bunge la Katiba ambayo imewajali kwa kuwekwa vipengele muhimu kwao.
 Wazee wa kimila wa kabila la kihehe wakimvisha mgogole Kinana kwa kutambua mchango wake nchini
 Kinana akipatiwa mkuki kwa ajili ya kujilinda dhidi ya maadui
 Kinana akimkabidhi kadi ya CCM mwanachama mpya aliyejiunga katika mutano huo
Kinana akisalimiana na wananchi baada kumaliza kuhutubia mkutano

Post a Comment

Previous Post Next Post