CHELSEA
imeamua kupeleka nguvu zake kumfukuzia sentahafu kinda wa Stuttgart ya
Ujerumani, Antonio Rudiger atakayerithi mikoba ya nahodha wao John
Terry.
Kwa
mujibu wa gazeti la The Star, The Blues inaamini beki huyo wa kati
mwenye umri wa miaka 21, ni chaguo sahili mbadala wa kipaumbele namba
moja katika usajili ujao, Raphael Varane, kwa sababu dau lake ni dogo,
karibu pauni milioni 7.
Inadaiwa
kuwa Chelsea imeamua kugeuzia kibao kwa Rudiger baada ya Real Madrid
kutaka pauni milioni 40 ili kuruhusu beki wake huyo kuondoka Santiago
Bernabeu.
Hata
hivyo, Stuttgart haionekana kuwa na mpango wa kumwachia Rudiger, baada
ya Mkurugenzi wake wa Michezo, Jochen Schneider, kueleza klabu yake
inafanya juu chini kujaribu kumbakisha sentahafu huyo kwa muda mrefu.
“Lengo letu ni kuongeza mkataba mrefu na Antonio Rudiger, Schneider ameliambia gazeti la Ujerumani la Bild.
Post a Comment