STAA wa Barcelona, Gerard Pique ameingia matatani baada ya kuwaambia polisi “mnanionea wivu kwa sababu mimi ni maarufu”.
Pique
alisimamaishwa na trafiki wakati akiendesha gari kuelekea casino akiwa
na kaka yake Jumapili iliyopita, na akatakiwa kutoka kwenye gari.
Alitekeleza amri hiyo, lakini akawaadhibu askari hao kwa kauli yake hiyo
ya kuudhi.
Kwa
mujibu wa gazeti la La Vanguardia, beki huyo wa zamani wa Manchester
United aliwatolea kauli hiyo tariki baada ya kumlima faini.
“Nitampigia
bosi wenu na atamaliza tatizo hili,” alikaririwa akisema staa huyo
kabla ya kukunjakunja karatasi (ya faini) na kuwatupia usoni.
Baadae Pique aliomba radhi kupitia ukurasa wake wa Twitter, lakini bado anakabiliwa na mashtaka mahakamani.
Post a Comment