Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi Prof. Idrissa Mshoro akiwaeleza waandishi
wa habari (Hawapo pichani) kuhusu mpango wa chuo hicho wa kuendelea na
jitihada za kutatua tatizo la udhibiti wa maji taka na tanga ngumu
ikiwemo ujengaji wa miundombinu ya majaribio ya teknolojia za kibiolojia
zinazobadili tanga ngumu au maji taka ambayo huzalishwa majumbani kuwa
mboji na gesi asili ya kupikia, wakati wa mkutano na waandishi wa habari
leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma wa
chuo hicho Prof. Gabriel Kassenga.
Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Ardhi ambaye pia ndiye mtaalam wa teknolojia za
kibiolojia zinazobadili tanga ngumu au maji taka (waste treatment
facilities) Dkt. Shabaan Mgana Akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo
pichani) namna Teknolojia hiyo ya kubadili taka ngumu na maji taka
inavyotumika na kuwasaidia wananchi walioonesha nia ya kuitumia ikiwamo
kupata mboji kwa ajili ya mazao, mimea pamoja na kupata gesi asili ya
kupikia, ambapo mpaka sasa kiasi cha nyumba 100 za awali katika mtaa wa
Migombani, kata ya Segerea na nyumba mia moja katika Chuo Kikuu cha
Ardhi zimeshaunganishwa katika Mradi huo, wakati wa mkutano na waandishi
wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho
Prof. Idrissa Mshoro.
Mkemia
Mkuu wa Kiwanda cha Mansoor Daya Chemicals Bw. Benedict Mtenga
Akiwaeleza waandishi wa habari(hawapo pichani) jinsi wanavyoendelea
kunufaika na teknolojia hiyo ya kibiolojia ikiwemo kutumika kusafisha
maji taka yanayozalishwa na kiwanda hicho na kuepusha uharibifu wa
mazingira,wakati wa ziara iliyofanywa katika kiwanda hicho ili kuona
jinsi teknolojia inavyofanya kazi.
Miundombinu
ya majaribio ya teknolojia za kibiolojia zinazobadili tanga ngumu au
maji taka ambayo huzalishwa majumbani kuwa mboji zilizojengwa katika
maeneo ya Chuo Kikuu cha Ardhi, mtaa wa Migombani, kata ya Segerea na
katika kiwanda cha Madawa ya Binadamu cha Mansoor Daya Chemicals.
Baadhi
ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo na kutembelea maeneo
ilipojengwa miundombinu ya teknolojia za kibiolojia zinazobadili taka
ngumu au maji taka ambayo huzalishwa majumbani kuwa mboji.
Mwanafunzi
wa Chuo Kikuu cha Ardhi Bi. Minza Selele akiwaeleza waandishi wa habari
jinsi mtambo wa kuzalisha gesi asili inayotokana na mabaki ya chakula,
taka za jikoni na mbogamboga, wakati wa ziara iliyofanywa chuoni hapo
kujionea jinsi teknolojia ya kubadili taka ngumu na kuzalisha gesi asili
ya kupikia inayofanya kazi.
Mwanafunzi
wa Chuo Kikuu cha Ardhi Bi. Minza Selele akiwasha karatasi kwa kutumia
Gesi Asili iliyozalishwa na Mtambo huo.(Picha na Hassan Silayo-MAELEZO).
Post a Comment