Taasisi ya kuthibiti magonjwa nchini Marekani CDC
Virusi
vya ugonjwa wa Ebola huenda vimedhibitiwa nchini Nigeria na
Senegal,kulingana na maafisa wa afya nchini Marekani,baada ya visa
vipya kutoripotiwa katika mataifa hayo kwa kipindi cha mwezi mmoja sasa.
Taasisi
ya kudhibiti magonjwa nchini Marekani CDC imesema kuwa mlipuko wa
ugonjwa huo unaweza kutangazwa kwamba umeisha nchini Nigeria ifikiapo
mwezi ujao.
Hatahivyo ugonjwa huo unaendelea kuathiri maisha ya
raia wengi katika maeneo mengine ya Afrika Magharibi hususan
Liberia,Guinea na Sierra Leone.
Shirika la afya duniani WHO
linasema kuwa zaidi ya watu 3000 wamefariki kutokana na ugonjwa huo
kufikia sasa wengi wakitoka nchini Liberia.
Mlipuko huo ndio hatari zaidi kuwahi kutokea katika historia ya ugonjwa huo.
Afisa wa CDC Tom Frieden
Mkuu wa Umoja wa Mataifa
anayesimamia kitengo cha kukabiliana na ugonjwa huo amesema kuwa hatua
kubwa zitapigwa katika kipindi cha siku sitini zijazo kuuthibiti ugonjwa
huo.
Mlipuko wa ugonjwa huo katika mataifa ya Nigeria na Senegal
umekuwa mdogo ikilinganishwa na mataifa mengine ya Afrika Magharibi huku
visa 20 vikithibitishwa kwa jumla kati ya mataifa hayo mawili.
Nchini
Nigeria ,ambalo ndio taifa lenye idadi kubwa ya watu barani
Afrika,kumekuwa na visa 19 vya ugonjwa huo ambavyo vimethibitishwa
pamoja na vifo vinane tangu kisa cha kwanza kugunduliwa mnamo mwezi
Julai.
Kisa cha mwisho kuripotiwa nchini humo kilikuwa kile cha tarehe 5 mwezi Septemba kulinga na CDC.


إرسال تعليق